Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

Monday, January 2, 2017

KIPA WA SIMBA ALIVYOCHAFUA DAFTARI


Golikipa wa Simba Daniel Agyei ameruhusu nyavu zake kutikiswa kwa mara ya kwanza tangu alipojiunga na klabu hiyo katika dirisha dogo la usajili kuchukua nafasi ya Vicent Angban ambaye baadae alitemwa kwa kile kinachotajwa kuwa ni kiwango kidogo.
Agyei amecheza mechi tatu za ligi kuu Tanzania bara (Ndanda  FC 0- Simba, Simba 1-0 JKT Ruvu na Ruvu Shooting 0-1 Simba) na akifanikiwa kutengeneza clean sheets kwenye mechi zote. Alicheza pia mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya Mtibwa Sugar (haukua mchezo wa mashindano rasmi) na kumaliza dakika 90 akiwa ameruhusu magoli mawili Simba ilipoteza kwa kufungwa 2-1.
Goli alilofungwa golikipa huyo kutoka Ghana lilitokana na kona ambapo beki wa Simba Novat Lufunga alijifunga wakati akipambana kuokoa mpira.
Kwahiyo Agyei ameruhusu goli moja hadi sasa katika mashindano rasmi yanayotambuliwa na TFF ukiondoa mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo aliruhusu magoli mawili katika kipigo cha Simba 1-2 Mtibwa Sugar.
Chanzo: http://shaffihdauda.co.tz/2017/01/01/golikipa-wa-simba-amechafua-daftari/
[Continue Reading]

Tuesday, March 31, 2015

List ya Wanasoka na Makocha Tajiri Dunia,

List ya wachezaji matajiri ambayo imetolewa na Jarida la soka la nchini Ufaransa limetoa orodha ya wanasoka na makocha wenye utajili mkubwa kwasasa ulimwenguni,orodha hiyo kwa upande wa wanasoka inaongozwa na Lionel Messi ikifuatiwa na mpinzani wake Criastiano Ronaldo, utajili huo wa Messi unatokana na jumla ya pesa zote anazozipata kutokana na mshahara pamoja na mikataba aliyosaini na makampuni mbali mbali.

 


Kwa upande wa makocha Mreno Jose Mourinho akashika nafasi ya kwanza akiwa kampiga gepu Carlo Ancelotti kwa Euro 1.8 Million akiwa ni kocha wa Chelsea.


[Continue Reading]

Thursday, November 13, 2014

JONAS MKUDE ASAINI MIAKA MIWILI SIMBA


Hatimaye kiungo Jonas Mkude amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba.
Mkude ambaye ni tegemeo katika kiungo cha ulinzi cha Simba, amesaini mkataba huo leo mbele ya Rais wa Simba, Evans Aveva.
Pamoja na Aveva na viongozi wengine wa Simba akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, Mkude alisaini mkataba huo mbele ya waandishi wa habari. Awali kulikuwa na taarifa kwamba Mkude ameishaongeza mkataba Simba.
[Continue Reading]

Wednesday, August 6, 2014

YANGA WAISHANGAA CECAFA

Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu ya Yanga, kushoto kwake ni Kocha Mkuu Marcio Maximo na afisa habari Baraka Kizuguto



Uongozi wa klabu ya Young Africans leo umefanya mkutano na waandishi wa habari nchini na kusema kilichofanywa na waandaji wa michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuiondoa timu isishiriki ni cha kushangaza sana na kinadidimiza soka kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema walipata barua ya mwaliko wa kushiriki mashindano tarehe 25/7/2014 na kudhibitisha kushiriki michuano hiyo siku hiyo hiyo kwa kuandika barua iliyokwenda TFF na kisha wao kuiwasilisha kwa CECAFA.
"Baada ya kudhibitisha kushiriki michuano hiyo tuliambiwa na CECAFA tutume orodha ya wachezaji na viongozi ambao watasafiri kuelekea nchini Rwanda kwenye michuano hiyo ili waweze kuandaa tiketi za ndege na sehemu ya malazi kitu ambacho tulitimiza" alisema Beno. 
Lakini katika hali ya kushangaza jana tulipokea barua kutoka TFF ikisema CECAFA imetuondoa kwenye mashindano hayo kwa kushindwa kukidhi vigezo na kuiteua timu ya Azam kuchukua nafasi yetu "aliongeza Beno."
Kanuni za CECAFA zipo wazi kuwa wachezaji wanaopaswa kushiriki michuano hiyo ni lazima wawe na leseni za kucheza mpira kutoka kwa chama husika, jambo ambalo katika orodha tuliyowapelekea wachezaji wote wataichezea Yanga msimu huu wa 2014/2015.
Kocha Marcio Maximo alianza maandalizi ya kikosi ambacho kingekwenda kushiriki michuano hiyo ambayo ilipaswa kuanza ijumaa tarehe 8/8/2014 kwa Yanga kufungua dimba la wenyeji timu ya Rayon FC .
Kikosi ambacho kocha mkuu alikichagua kwenda kwenye michuano ya Kagame kilikua na jumla ya wachezaji 20, 15 wakiwa kutoka timu ya kikosi cha wakubwa na wachezaji watano wakitoka kikosi cha pili U20 chini ya kocha Leonado Neiva ambaye amekua na wachezaji hao kwa takribani mwezi mmoja.
Lakini walichokiamua CECAFA ni kuiondoa klabu ya Yanga na kuipa nafasi timu nyingine kwa kusema kikosi kilichopelekwa hawakubaliani nacho na hata kocha mkuu Marcio Maximo haendi, hao ndo tulipojua ya kuwa wanataka majina ya watu na sio timu.
Zifuatazo ni sababu za Kiufundi ambazo Yanga ilizipelekea CECAFA kuhusu kikosi hicho kutojumuisha wachezaji wa timu za Taifa.
a) Ripoti ya kocha aliyeondoka Yanga msimu uliopita Hans ilitoa maelekezo ya kupunguza wachezaji tisa (9) na wachezaji wawili kujiunga na klabu ya Azam hivyo kufanya kikosi kupungua wachezaji 11 kutoka katika idadi ya wachezaji 30 wa msimu uliopita.
b) Wachezaji 10 wa Yanga wamekuwa na majukumu ya timu za Taifa za Tanzania (Taifa Stars), Rwanda na Uganda tangu Aprili 19, 2014 mpaka mwanzoni mwa Agosti, takribani miezi mitatu wamekuwa kambini bila kupata muda wa kupumzika.
c)  Benchi la Ufundi la Yanga ni jipya kuanzia kocha mkuu Maximo na wasaidizi wake watatu Leonardo Neiva, Salavatory Edwarda na Shadrack Nsajigwa hivyo wanahitaji muda wa kuwajua wachezaji waliokuwa kwenye timu ya Taifa ndo maana hawakuwajumuisha kwenye kikosi cha kwenda Kigali Rwanda.
d)  Baadhi ya wachezaji wanahitaji Vibali vya kufanyia kazi nchini, uhamisho wa Kimataifa (ITC) ili waweza kushiriki michuano ya Kagame, na moja ya kanuni za CECAFA mchezaji anayeshiriki mashindano hayo ni lazima awe na leseni ya kucheza mpira kwa ligi ya ndani.
e) Katika wachezaji 20 waliochaguliwa kushiriki michuano ya Kagame, wachezaji 6 wamepandishwa moja moja katika kikosi cha wakubwa msimu huu hivyo kufanya idadi ya wachezaji wa U20 kuwa watano tu.
f) Wachezaji walikokuwa kambini Taifa Stars kwa takribani miezi mitatu bila ya kupumzika, daktari alipendekeza wapate japo siku kumi na nne (14) za kupumzika ili miili yao iweze kupoa na kuanza upya tena maandalizi ya msimu mpya.
g) Yanga tunaamini hakuna mtu yoyote zaidi ya Kocha Mkuu anayeweza kutupangia kikosi cha kwanza, sababu yeye ndio anayekaa na wachezaji mda wote na kujua ubora wa wachezaji wake.
[Continue Reading]

Saturday, July 5, 2014

VIJANA WA JANGWANI NI MWENDO MDUNDO NA TIZI LA MCHANGANI


 Wachezaji wa Timu ya Yanga wakiendelea kujifua kwa nguvu zote kwenye Ufukwe wa Bichi ya Barabara ya Ocean Rodi jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi,ikiwa ni katika maandalizi ya mashindano ya ligi kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi hapo Agosti 24 2014.Timu ya Yanga ipo chini ya Kocha aliewahi kuinoa Timu ya Taifa "Taifa Stars" miaka ya nyuma,Kocha Marcio Maximo (wa pili kulia) akiwa na msaidizi wake Leonado Neiva (wa nne kulia) pamoja na Mchezaji wa zamani wa timu hiyo,Salvatory Edward (kulia).Picha zote na Othman Michuzi.

Kocha Marcio Maximo akimueleza jambo mmoja wa Wasaidizi wake ambaye ni Mchezaji wa zamani wa timu ya Yanga,Salvatory Edward.

Kocha Msaidizi wa Timu ya Yanga,Leonado Neiva akitoa maelekezo kwa wachezaji wa Timu ya Yanga,wakati wa Mazoezi yao yaliyoendelea kufanyika leo kwenye Ufukwe wa Bichi ya Barabara ya Ocean Rodi jijini Dar es Salaam.

Kiungo Mshambuliaji wa Timu ya Yanga kutoka nchini Brazil,Andrey Coutinho akishiriki kwenye mazoezi hayo.Kulia ni Mmoja wa Magolikipa wa timu hiyo,Ally Mustafa.

[Continue Reading]

HIZI NDIO PICHA JINSI NEYMAR ALIVYOVUNJIKA UTI WA MGONGO







Mashabiki wa timu ya taifa ya Brazil wakiwa nje ya hospital ya SAO CARLOS ili kujua hatma ya mshambuliaji wao hatari Neymar Jr
[Continue Reading]

Saturday, June 7, 2014

FAHAMU WACHEZAJI WATAKAO KOSA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA HUKO BRAZIL

Players injured out of World Cup:
Reus
Ribery
Falcao
Montes
Valdes
Thiago
Gundogan
El Shaarawy
Walcott
Rossi
Montolivo
Strootman
Benteke
[Continue Reading]

Friday, June 6, 2014

Kapombe amuonyesha jeuri Mrisho Ngassa Jangwani

Shomari Kapombe akiwa mazoezini na timu ya Azam.PICHA|MAKTABA 
NI uhakika asilimia 100 kwamba kiraka, Shomari Kapombe, ni mali ya Azam FC. Lakini kuna kitu kimoja kimemtokea mchezaji huyo ambacho kimeonyesha kwamba yeye ni jeuri na ana thamani kuliko Mrisho Ngassa wa Yanga.
Timu tajiri zaidi Tanzania na pekee Afrika Mashariki na Kati yenye uwanja binafsi ulioidhinishwa kwa michuano ya kimataifa, Azam FC, imenasa saini ya Kapombe kwa dau la Euro 47300 (Sh105 milioni).
Dau hilo la Kapombe limefuta rekodi ya Ngassa ambaye alikuwa mchezaji ghali zaidi wa kibongo kwenye Ligi ya Bara. Ngassa aliweka historia hiyo alipohamishwa kutoka Yanga kwenda Azam kwa dau la Sh 98 milioni mwaka 2010 kabla kwenda Simba kwa mkopo na baadaye kurudi Jangwani kwa dau la kawaida.
Kati ya kiasi hicho cha fedha za Kapombe, Euro 43000 (Sh95.8 milioni) zimeenda kwa klabu ya AS Cannes ya Ufaransa iliyokuwa na mkataba naye halafu asilimia 10 yaani Euro 4,300 (Sh9.5milioni) zitapelekwa Simba ikishapata uongozi mpya.
Chanzo makini cha Mwanaspoti ndani ya Azam, kilisema: “Tumeshatoa kiasi hicho cha fedha na sasa Kapombe yupo huru kuvaa jezi za Azam msimu ujao, hizo fedha za Simba zitachukuliwa na uongozi mpya utakaoingia madarakani kwani sasa tunawaacha waendelee na uchaguzi wao.”
Kabla ya usajili huo, Kapombe alianza kuonekana katika viwanja vya Azam Complex vilivyopo Chamazi, Mbagala jijini Dar es Salaam akifanya mazoezi na jezi za timu hiyo na kuamsha hisia kwamba atajiunga na mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita.
Ingawa Simba waliona hali hiyo wakapuuzia wakidhani ni masihara na kwamba kijana atarudi tu Msimbazi bila presha.
Kwa uhamisho huo, Kapombe anayemudu kucheza nafasi zote za ulinzi na kiungo katika timu, atavaa jezi ya Azam katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na ile ya Kombe la Kagame na ligi kuu. 
Huu ni usajili wa tano wa Azam baada ya hivi karibuni kuwasajili wachezaji wawili waliomaliza mkataba na Yanga ambao ni Didier Kavumbagu na Frank Domayo. Wengine waliosajiliwa na Azam hadi sas ni Ismail Diara wa Mali na Abdallah Kheri Salum kutoka Zanzibar.
Chanzo: Mwanaspoti
[Continue Reading]

Sunday, June 1, 2014

JOSEPH MINALA ANA MIAKA 17 NA SI 42:SOMA HAPA KUJUA KINACHOENDELEA KUHUSU MWANANDINGA HUYU

20140529-135211-49931047.jpg 
Hatimaye kitendawili cha umri wa msakata ndinga wa Lazio, Joseph Minala kimeteguliwa kwa kuhakikishwa kwamba umri wake ni miaka 17 si 42 iliyodaiwa na Tovuti ya Soka ya Afrika.

Kiungo huyo alikuwa akichunguzwa na Chama cha Soka Italia baada ya yeye kudai ana umri wa miaka 17 lakini usoni akaonekana kuwa na makunyanzi kama mtu aliyevuka sana umri huo. Wataalamu wanasema kwamba ‘uzee’ unaonekana usoni mwake kwa sababu ya maisha ya dhiki siku zilizopita.
Minala alizaliwa Cameroon na alijiunga na klabu hiyo ya jijini Roma msimu uliopita wa kiangazi na kuwachezea katika mashindano ya vijana Februari mwaka huu, huku watu wengi wakishangaa ikiwa kweli ni kijana.

Lazio walikuwa wametishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya yeyote aliyekwua akihoji uhalali wa mchezaji wao huyo kushiriki mashindano hayo na pia dhidi ya madai kwamba ana umri wa miaka 42, yaani miaka 25 zaidi ya umri wake halali.

Klabu hiyo imesema kwamba imepata hata cheti chake cha kuzaliwa ambacho walikipeleka kwenye chama cha soka na baada ya hapo watashughulika na yeyote atakayeendeleza propaganda za kumchafua kijana huyo juu ya umri wake.
Mtandao huo ulidai kwamba Minala alikiri kuwa umri wake wakati huo ulikuwa miaka 41 na hivyo sasa amefikisha 42 lakini yeye anakana kuzungumza na watu wa tovuti iliyotoa habari hizo.

“Usoni mwake kuna alama au dalili za maisha yake ya nyuma, ambayo hayakuwa mazuri. Ni hivyo tu. Hakuna kitu kingine chochote kinachoweza kumtonya mtu kwamba eti ana miaka zaidi ya 40. Ukiangalia kichwa chake ni cha kijana.

“Lakini acheza kwa kasi sana hata anapozungukwa na wachezaji wengi, mchezaji wa umri huo hangeweza kuwa na makeke kama huyu,” anasema mwanahabari Max Evangelista ambaye ni Mtaliano.
Minala anaelezwa kwamba ni yatima na aliishi maisha ya tabu sana mitaani nchini mwake kabla ya kupelekwa kituo cha watoto yatima kabla ya kubahatika kucheza soka barabarani kisha akapelekwa kwenye viwanja, akapanda chati hadi kupelekwa Italia.
[Continue Reading]

Wednesday, May 28, 2014

TETESI ZA SOKA KWENYE MAGAZETI YA UINGEREZA NA TOVUTI ZA ULAYA

Boss mpya wa Tottenham Mauricio Pochettino anataka kumchukua nahodha wake wa zamani Adam Lallana (Guardian), Chelsea bado wanamnyatia Rafael Varane kutoka Real Madrid kuziba pengo la David Luiz (Daily Star), Edin Hazard amefutilia mbali taarifa kuwa anataka kwenda PSG (London Evening Standard), Man United wanamfuatilia kiungo wa PSG Adrien Rabiot, ambaye pia ananyatiwa na Arsenal, Chelsea na Man City (Daily Mail), Harry Radknapp Wa QPR amekiri kuwa itakuwa ngumu kutomzuia Loic Remy kuondoka- Liverpool, Arsenal na Chelsea wameonesha nia ya kumtaka (Daily Express), Chelsea wamekubali kumsaini tena Tiago kutoka Atlètico Madrid (Daily Mail), Arsene Wenger huenda akamchukua tena Kim Kallstrom kwa mkopo (Daily Mirror), Niklas Bendtner anasakwa na timu nne baada ya kutoswa na Arsenal- Leicester City, Burnley, Crystal Palace na Hull City (Sun), Monaco wanamtaka Alexander Kolarov Wa Man City (Sun), Chelsea wapo tayari kulipa paundi milioni 19.4 kumchukua beki wa kushoto wa Atlètico Madrid Filipe Luis (Marca).
NA HATIMAYE.. Kitabu kipya kilichotoka kinasema striker wa Real Madrid na Ureno, Cristiano Ronaldo ana mfupa wa ziada kwenye mkuu wake wa kulia unaomsaidia katika kupiga free kick au zuruba, limeandika The Sun. Share tetesi hizi na wapenda soka wote. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa


chanzo Salim Kikeke

[Continue Reading]

Saturday, May 17, 2014

YANGA KIMENUKA MASTAA KIBAO KUPUKUTISHWA


Kipa Juma Kaseja akiwa na cheti chake cha ukocha alichotunukiwa jana Ijumaa baada ya kuhitimu mjini Morogoro. Picha na Juma Mtanda 
YANGA iko kwenye taratibu za kuachana na wachezaji wake mahiri ambao kuna uwezekano mkubwa wakatua Simba kwani baadhi yao wameshafanya mazungumzo ya awali Msimbazi. Wachezaji hao ni kiungo mwenye nguvu Athuman Idd ‘Chuji’, David Luhende, Juma Abdul na Ally Mustapha ‘Barthez’.
Lakini cha kushtua zaidi kipa mwenye heshima kubwa na rekodi ya aina yake nchini, Juma Kaseja yuko katika mazungumzo na uongozi wa Yanga akiwashawishi kusitisha mkataba wake wa mwaka mmoja kwa kile alichodai kwamba hana bahati na timu hiyo kwa sasa.
Kaseja ambaye hakuwa na wakati mzuri msimu uliopita jana Ijumaa alifuzu kozi ya awali ya ukocha na kupata alama ya daraja A katika mafunzo yaliyoanza Mei 5 mwaka huu katika Manispaa ya Morogoro.  
Habari za uhakika kutoka kwenye kamati ya usajili zinasema Chuji anaachwa kutokana na nidhamu ndogo ingawa baadhi wanapinga na kusema kwamba ni mbadala mzuri wa Frank Domayo aliyesaini Azam.
Mbali na Chuji pia klabu hiyo imewachomoa Luhende na Abdul ambao awali waliudengulia uongozi wa klabu hiyo kuongeza mkataba huku Luhende ikiripotiwa kuwa amefanya mazungumzo na Simba ingawa hawana mpango nae sana kwavile aliwaringia awali wakafanya mazungumzo na Abdi Banda wa Coastal Union. Uongozi wa Simba umekiri kufanya mazungumzo na Barthez na watamalizana muda wowote.
Habari kutoka kwenye kamati ya usajili ya Yanga zinasema kuwa zaidi ya nusu ya wachezaji inaowahitaji imeshawapa mikataba mipya ambapo mchezaji wa mwisho alikuwa Mbuyu Twite. Kamati hiyo imepanga kupeleka baadhi ya wachezaji wenye mikataba kwa mikopo kwenye klabu zingine za Bara.
“Luhende Simba walimuhitaji kwa ada ya usajili ya Sh 6 Milioni na aichezee klabu hiyo ya Msimbazi kwa miezi sita lakini akagoma, alitaka aongezewe dau zaidi na Yanga pia aligoma kusaini yeye na Juma Abdul wote walikuwa mkumbo mmoja na Frank Domayo na Didier Kavumbagu,” kilisema chanzo chetu.
Habari za ndani zinadai kwamba Yanga ipo mbioni kuingia mkataba na Kelvin Edward wa JKT Ruvu na pia imepanga kuibomoa Mtibwa Sugar ingawa bado haijawekwa wazi ni kifaa gani.
Katika hatua nyingine, Mwanaspoti linajua kwamba mpaka jana Ijumaa Yanga ilikuwa imebaki na majina ya makocha watatu ambao ni kutoka katika nchi za Brazil, Uholanzi na  Ujerumani. Habari zinasema kwamba majina ya makocha hao yapo kwa Mwenyekiti Yusuf Manji ambaye ndiye atakayefanya uamuzi wa mwisho kwani tayari kocha Hans Pluijm ameshatoa sifa za makocha hao kabla hajaondoka alfajiri ya leo Jumamosi.
Makocha hao imeripotiwa kwamba mmoja wao anafanya kazi nchini Ghana na ana uzoefu mkubwa na mazingira ya Kiafrika ambapo atatua nchini na mchezaji mmoja anayecheza nafasi ya kiungo.
Credit;Mwanaspoti
[Continue Reading]

Thursday, May 15, 2014

Taarifa kuhusu kutangazwa kwa kocha mpya wa Man Utd

giggs-van-gaalWiki kadhaa baada ya kumtimua kocha David Moyes klabu ya Manchester united wanakaribia kumtangaza kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi Louis van Gaal kuwa meneja mpya wa timu hiyo.
Mholanzi huyo tayari ameshakubali kuchukua madaraka ya ukocha Old Trafford lakini bado ana kazi ya kuiongoza Uholanzi kwenye michuano ya kombe la dunia na maandalizi ya kujiandaa na michuano hiyo yamesababisha dili lake na United kuchelewa kukamilika.
Mwanzoni iliripotiwa kwamba angetambulishwa mwishoni mwa wiki hii lakini badala yake ameendelea kubaki nchini Uholanzi na inaaminika sasa atatambulishwa wiki ijayo baada ya mchezo wa kirafiki.
Jana Ryan Giggs ambae ameshika madaraka ya ukocha kwa muda alisafiri mpaka Uholanzi ambapo alikutana na Van Gaal mjini Noordwijk kwa ajili ya kuzungumza juu ya Giggs kupewa madaraka ya kocha msaidizi pamoja na mipango ya usajili msimu ujao.
Chanzo;Millardayo
[Continue Reading]

Wednesday, May 14, 2014

SOMA HAPA WACHEZAJI WATAOIWAKILISHA TIMU YA TAIFA YA UHOLANZI KWENYE MASHINDANO MAKUBWA YA KOMBE LA DUNIA


Netherlands squad
Goalkeepers: 
Jasper Cillessen (Ajax), Tim Krul (Newcastle United/ENG), Michel Vorm (Swansea City/ENG), Jeroen Zoet (PSV Eindhoven)
Defenders: Patrick van Aanholt (Vitesse Arnhem), Daley Blind (Ajax), Daryl Janmaat, Terence Kongolo, Bruno Martins Indi (all Feyenoord), Karim Rekik (PSV Eindhoven), Joël Veltman (Ajax), Paul Verhaegh (Augsburg/GER), Ron Vlaar (Aston Villa/ENG), Stefan De Vrij (Feyenoord)
Midfielders: Jordy Clasie (Feyenoord), Leroy Fer (Norwich City/ENG), Jonathan De Guzman (Swansea City/ENG), Nigel de Jong (AC Milan/ITA), Wesley Sneijder (Galatasaray/TUR), Tonny Vilhena (Feyenoord), Rafael van der Vaart (Hamburg/GER), Georginio Wijnaldum (PSV Eindhoven)
Forwards: Jean-Paul Boëtius (Feyenoord), Memphis Depay (PSV Eindhoven), Klaas-Jan Huntelaar (Schalke 04/GER), Dirk Kuijt (Fenerbahce/TUR), Jeremain Lens (Dynamo Kiev/UKR), Robin van Persie (Manchester United/ENG), Arjen Robben (Bayern Munich/GER), Quincy Promes (FC Twente)
[Continue Reading]

SOMA HAPA WACHEZAJI WATAOIWAKILISHA TIMU YA TAIFA YA UFARANSA KWENYE MASHINDANO MAKUBWA YA KOMBE LA DUNIA


France squad
Goalkeepers: 
Hugo Lloris (Tottenham), Steve Mandanda (Marseille), Mickael Landreau (Bastia)
Defenders: Mathieu Debuchy (Newcastle), Bacary Sagna (Arsenal), Laurent Koscielny (Arsenal), Mamadou Sakho (Liverpool), Raphael Varane (Real Madrid), Eliaquim Mangala (Porto), Patrice Evra (Manchester United), Lucas Digne (PSG)
Midfielders: Yohan Cabaye (PSG), Clement Grenier (Lyon), Blaise Matuidi (PSG), Rio Mavuba (Lille), Paul Pogba (Juventus), Moussa Sissoko (Newcastle), Mathieu Valbuena (Marseille)
Forwards: Karim Benzema (Real Madrid), Olivier Giroud (Arsenal), Antoine Griezmann (Real Sociedad), Franck Ribery (Bayern Munich), Loic Remy (QPR)
Standby: Remy Cabella (Montpellier), Maxime Gonalons (Lyon), Alexandre Lacazette (Lyon), Loic Perrin (Saint-Etienne), Stephane Ruffier (Saint-Etienne), Morgan Schneiderlin (Southampton), Benoit Tremoulinas (Bordeaux)
[Continue Reading]

Tuesday, May 6, 2014

Sare ya 3-3 yamliza Luis Suarez

Luis Suarez alia baada ya Liverpool kwenda sare ya mabao matatu na Crystal Palace
Liverpool wameona giza huku kombe la Ligi ya Premier likiwakwepa baada ya kwenda sare ya mabao matatu dhidi ya Crysral Palace .
Cha kushangaza ni kwamba Liverpool walikuwa mbele kwa mabao matatu lakini Cyrstal walitifua kivumbi na kutoka nyuma bila bao huku wakimaliza mechi kwa mabao matatu sawa na Liverpool.
Joe Allen, Daniel Sturridge na Luis Suarez waliiweka mbele klabu yao katika muda wa saa moja kwa mabao matatu.
Lakini Damien Delaney na Dwight Gayle walipunguza pengo hilo na kuingiza mabao matatu katika muda wa dakika mbili katika kipindi cha pili cha mechi.
Hali hii iliwachaa mashabiki wa Liverpool vinywa wazi wasijuie cha kusema.
Liverpool sasa wako mbele ya Man City kwa poiti moja tu kwenye jedwali la alama.City bado wako na mechi moja kucheza.
City watamenyana na Aston Villa katika uwanja wa Etihad mnamo siku ya Jumatano, kabla ya kumaliza msimu kwa mechi nyingine dhidi ya West Ham Jumapili.
[Continue Reading]

Cole aaga Stamford Bridge huku akilia

Cole 
NI mwisho wa zamani. Hakuna marefu yasiyo na mwisho. Juzi Jumapili inaweza kuwa siku ya mwisho kwa beki wa kushoto wa Chelsea, Ashley Cole, kuvaa jezi katika Uwanja wa Stamford Bridge baada ya nyota huyo kuondoka uwanjani hapo akiwa analia.
Cole, 33, alimwaga machozi wakati akiwaaga mashabiki wa Chelsea baada ya pambano la mwisho la Chelsea uwanjani Stamford Bridge dhidi ya Norwich City katika msimu huu wa Ligi Kuu England, mechi hiyo ilimalizika kwa timu hizo kutofungana.
Wiki ijayo Chelsea itacheza mechi ya mwisho ya msimu dhidi ya Cardiff City lakini itakuwa ugenini. Baada ya mechi dhidi ya Norwich, wachezaji wa Chelsea walizunguka uwanja wakiwaaga mashabiki wao na ndipo Cole alipoangua kilio kwa uchungu.
Baadaye beki huyo alibembelezwa na nyota wengine wawili wa Chelsea, Frank Lampard na John Terry, ambao nao hawana uhakika wa kuendelea kuwepo katika kikosi cha Chelsea msimu ujao baada ya kupoteza namba.
Cole amepoteza nafasi yake Chelsea baada ya kuporwa namba na Mhispaniola, Cesar Azpilicueta, ambaye licha ya kuanzia maisha yake katika upande wa kulia, alihamishiwa upande wa kushoto na kocha, Jose Mourinho na amekuwa akifanya vyema.
Cole mkataba wake utamalizika mwishoni mwa msimu huu na atakuwa huru kujiunga na timu yoyote anayotaka baada ya Chelsea kushindwa kumpatia mkataba mwingine.
Cole alijiunga Chelsea mwaka 2006 katika uhamisho uliokuwa na utata mkubwa, tangu hapo ameichezea Chelsea zaidi ya mechi 200 kwa mafanikio akitwaa ubingwa wa Ulaya, ubingwa wa Europa, mataji manne ya Kombe la FA na mawili ya Ligi Kuu England.
Kumekuwapo na uvumi kwamba nyota huyo amekuwa anatakiwa na Real Madrid ya Hispania huku pia akihusishwa kucheza katika Ligi Kuu Marekani ambako inadaiwa klabu ya New York Bulls inamhitaji.
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers, pia anadaiwa kumtaka beki huyo wa zamani wa Arsenal wakati huu upande wa kushoto wa timu hiyo ya Anfield ukiwa unalegalega tangu kuumia kwa Jose Enrique.
Chanzo Mwanaspoti
[Continue Reading]

Sunday, January 26, 2014

UNAFAHAMU NINI JUU HIZI NAMBA ZA JEZI KWENYE TIMU YA MAN UTD NA ATAKACHOKUTANA NACHO MCHEZAJI JUAN MATA BAADA YA KUSAINI MAN UTD

Timu ya Manchester Utd ya Nchini Uingereza yenye maskani yake katika Jiji la Manchester imemaliza uvumi uliokuwa umeenea juu ya Mchezaji Juan Mata  raia wa Spain aliyekuwa mchezaji wa timu ya Cheslea ya nchini Uingereza yenye maskani yake Jijini London.
Man Utd waliweza kumsani mchezaji kwa kitita cha £37.1million 
Mchezaji Juan Mata baada ya kusaini anaweza kukumbana na wakati mgumu juu ya Namba atayovaa kwenye jezi yake na hii ni List juu ya wachezaji waliowahi kupitia katika timu ya Manchester waliokuwa wakivaa jezi Namba 7,8 na 9 ambazo ameambiwa achague kama ataitaji

Jezi namba 7 hapo nyuma iliwahi kuvaliwa na
George Best
Eric Cantona
David Beckham
Christiano Ronaldo

Jezi namba 8 hapo nyuma iliwahi kuvaliwa na
Brian Kidd
Paul Ince 
Nick Butt
Wayne Rooney kabla ya kubadilishiwa na kupewa jezi namba 10

Jezi namba 9 hapo nyuma iliwahi kuvaliwa na
Sir Bobby Charlton
Andy Cole
Dimitar Berbatov

Unaweza kutoa Maoni yako Juu ya Namba itayomfaa Mchezaji huyo

[Continue Reading]

JUAN MATA AWAANDIKIA CHELSEA BARUA YA KUWAAGA MARA BAADA YA KUJIUNGA MAN U-VERY TOUCHING

On the completion of his transfer from Chelsea FC, Juan Mata took out time to write a letter to everyone associated with Chelsea. And yes, this is very emotional indeed. Get ready to board the feels train (an overused but appropriate phrase).

Juan Mata: “Hi everyone, As you can imagine this is a very important day in my life, and with these lines I would like to express the memories and emotions that come to me as I write. This letter is written from my heart, and first of all I would like to say that I will never forget all the affection given to me by the Chelsea fans. From the very first day until the last. With your support and affection I have grown up as a player and I have had an amazing time both on and off the pitch. I will always feel the gratitude towards you. Always. No words are enough to give back all the things I have received. There has been plenty of good moments: the FA Cup, my first trophy as a Blue; the immense happiness of winning titles for the first time in the club’s history, such as that magical Champions League night in Munich and the Europa League… On the other hand, I have experienced some complicated situations from a personal point of view, mainly during the last six months. Every message I got through the social media, every nice word you have said to me on the street, and of course, your support in the stadium, has made me feel incredibly proud of the Chelsea fans; you deserve a team like the one you’ve got, with so many fantastic players. I won’t forget the faith you put in me when I was given the player of the year award the last two seasons. I feel really proud and I will never forget those nights. Thank you so much for the way you have treated me, you have been unbelievable. I hope you understand that after going through a complicated and, for me, new situation in the last few months, I believe this is the best choice in order to carry on with my football career and to keep enjoying this sport. Before last summer, my intention was to stay here for a long time; as long as the club wanted me to, and to keep winning trophies for Chelsea FC. This is how happy I was in the club and in the city. However, as you all know, things changed after the preseason. From feeling like an important player, I started to experience some difficult situations and I felt unable to help the team to the extent that I wanted and was used to. Obviously, I fully respect the circumstances. Football is a team sport and it’s not easy to play regularly in such a good squad. In sports you may win or lose, but the most important thing is to give everything. I hope you know and feel that I have always done so. In every game, in every training session, without exception. I have always tried my best for the club. I would like to emphasise the affection, admiration and respect that I’ve had for my former team mates since the first day. I want to thank the captains for their help and understanding at all times. They made me feel comfortable when I arrived and they have supported me throughout the difficult times this season. I thank all my former team mates for these two and a half years and I wish them the best, personally and professionally, for the future. Of course I have been closer to some of them, but the most important thing is that my years in Chelsea have left me with great friends. Friends forever, football rivalries aside. I also want to highlight the day-to-day job of every member of the Chelsea staff: medical team, kit men, staff at Cobham and Stamford Bridge, media and marketing department, Chelsea TV team… All of them are very important in making this club a great one. Thank you for your treatment and your efforts to make the life of the players easier. Furthermore, thanks to every manager I have had the pleasure to work with during my time here. They have all been a big help for my progression as a player. I have always respected their decisions, whatever they were; they made me more mature and a stronger person. You learn from everything, and certain situations make you think about other team mates who are coping with similar situations more regularly. Thank you Andre for giving me the opportunity to join Chelsea FC. Without your support, none of this would have happened. To Robbie and Rafa, for their unlimited trust in me. And to Jose, for making me a stronger player, because in difficult moments, I have learnt to remain positive and to keep working hard. Lastly, I want to thank the Club, and in particular its owner, Roman Abramovich, for trusting me and making an important investment when signing me. Also for their understanding regarding my situation over the last months. I’m very glad to have been part of the squad that made his and our dream come true: winning the Champions League on that unforgettable night in Munich. Additionally, my years in Chelsea have been profitable for the club, which I’m very pleased about. I want to make clear that the stage that now comes to an end has been extremely important for me, personally and professionally. Although many of you, like myself, never thought this moment would come, this is football and a new chapter is about to begin. I would have liked to say good bye to all of you in the stadium, or in a press conference, but it has not been possible. I’m sure, i will be able to do it in the future, because is what you deserve. Evidently, today is a day of mixed feelings, remembering the past and looking forward to the future and what it has to bring. I look forward to being happy and to enjoy what I like the most: play football. I will never forget my time in Chelsea and the affection I take with me, I will keep forever. I wish you the best. A big hug to all of you. THANK YOU so much, Juan.”
[Continue Reading]
Powered By Blogger · Designed By Seo Blogger Templates