Showing posts with label STORI ZA MJINI. Show all posts
Showing posts with label STORI ZA MJINI. Show all posts

Saturday, December 27, 2014

MAJUTO: MASTAA WA KIKE WAMENIGEUZA BABU YAO!

Nguli wa sinema za Komedi Bongo, Amri Athuman ‘Majuto’ akiwa na Kajala Masanja.

Stori: Deogratius Mongela NGULI wa sinema za Komedi Bongo, Amri Athuman ‘Majuto’ amefunguka kuwa, mastaa wengi wa kike wamemgeuza babu yao kwa kumfanyia vituko kila wanapokutana naye.
Akitema mbili tatu na paparazi wetu baada ya kusambazwa kwa picha mtandaoni inayomuonesha akifanyiwa vituko  na staa mwenzake, Kajala Masanja, Mzee Majuto alisema watu wasimfikirie ndivyo sivyo kwani yeye wasanii wengi wa kike wamemgeuza babu yao.
Mzee Majuto akiwa na Odama.

“Wasanii wengi wamenizoea sana, huwa wananitania mara kwa mara na miye nawachukulia kama wanangu hasa hawa mastaa wa kike tofauti na wanaume, sijawahi kuwa na uhusiano na staa yeyote kati yao,” alisema Mzee Majuto.
[Continue Reading]

Sunday, December 21, 2014

Lulu:Kuwa Mama ni Heshima Sio Kuzeeka, Nipo Njiani

Mrembo na mwigizaji wa filamu hapa nchini, Elizabeth Michael “LULU” ameamua kufunguka na kusema mtazamo wake kuhusu swala la wasichana kuogopa/kukataa kuzaa kwakuofia kuwa watazeeka.

“Kwa akili Yangu ndogo... Nadhani kuwa Mzazi(Mama)ni heshima kubwa na Sio kuzeeka kama wasichana wengi wanavyofikiria....! Shout Out kwa Kila mwanamke aliyefanikisha kupata Heshima Hiyo...! Heshima kwa Mama wote Duniani ….Wengine Tuko njiani Inshallah”
Lulu aliweka bandiko hilo mtandaoni  baada yakuweka picha ya msanii  wamziki wa marekani, Ciara akiwa na mtoto wake wakiwa wamevalia kofia za “Christmas”.

Watu wengi walimpongeza kwa bandiko hili na hizi ni 'comment' kutoka kwa  Aunt Ezekieli na Zamaradi Mtetema.

Aunt Ezekiel:  Toka nimekufahamu leo ndio umeongea point toto akee... Kina mama Oyeeeeeee

Zamaradi Mtetema: Hasara.. baba yule!!! Hahahahaha uko tayari kwa ule mwendo!??

Lulu: @zamaradimketema ntauvumilia tu bwahahahahah

Na wewe ongeza yako hapo chini
[Continue Reading]

HATIMAYE SHILOLE AVISHWA PETE YA UCHUMBA NA NUH MZIWANDA JANA USIKU...TAZAMA PICHA HAPA


Mwigizaji na mwanamziki maarufu wa kike hapa Bongo, Zuwena Mohamed  “Shilole” ambae ni mama wa watoto wawili  usiku huu akishereke siku yake ya kuzaliwa maeneo ya Mikocheni jiji Dar, amevishwa pete ya uchumba na mpenzi wake wa muda mrefu sasa, Nuh Mziwanda ambae pia ni mwanamziki.
[Continue Reading]

Wednesday, December 3, 2014

Sheddy Clever alalamika jina lake kutoandikwa kwenye video mpya ya Diamond

Producer wa hits mbili za Diamond Platnumz ‘Number One’ na ‘Ntampata Wapi’ alionekana kufurahia mafanikio ya Diamond kwenye tuzo za Channel O, lakini kitu kimoja hakijakaa sawa moyoni mwake.




Sheddy amesema ameshangazwa baada ya kutoona jina lake likiandikwa kwenye video ya ‘Ntampata Wapi’.

“Biashara kweli ni matangazo na nilitakiwa niandikwe kweli kwenye ile video, lakini sasa kwa sababu imeshapita na vitu vingi vimeshatokea na ukiangalia kwenye video international wanafanya hivyo ila mpaka sasa hivi najaribu kujiuliza sijapata jibu kamili kwanini wanafanya hivyo,” Sheddy ameiambia E-News ya EATV.

“Ukiangalia video za West Africa za akina Davido, Wizkid wengi producer wa audio wanakuwa hawaandikwi kwenye video. Sasa sijui wanafuta ule mfumo wa wenzetu, sifahamu.”

[Continue Reading]

Sunday, November 30, 2014

SOMA ALICHOKISEMA MSANII ALI KIBA KUPITIA UKURASA WAKE WA FB


Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kufika leo siku yangu ya kuzaliwa Nov 29 na kuona mwaka mwengine.
Pia namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia kua na familia nzuri ninayoipenda na kuithamini sana - watoto wangu, kaka na dada zangu pamoja na wazazi wangu.
Ishaallah mwaka huu uwe wenye kheri na mafanikio mwengi.
Pia nawashukuru nyie mashabiki na wapenzi wa kazi yangu. Asanteni kwa kuni-wish. Mwenyezi Mungu awabariki sana. Ahsante sana.
-----
As I celebrate my birthday today Nov 29, I'd like to thank God for seeing another year. I also thank him for his abundant blessings particularly for my children, my loving brothers and sisters and for my amazing parents.
I pray that this year is filled with continued blessings and success.
I'm also grateful to God for you, my fans and for all your support. May he bless you all for all the love and support you have shown me. Thank you.
[Continue Reading]

DIAMOND PLATNUMZ AZIDI KUG'ARA, KUCHUKUA TUZO 3 ZA CHOAMVA 2014

November 29, haitakumbwa kwenye maisha ya Diamond Platnumz na familia yake pekee, bali pia kwenye muziki wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, baada ya hitmaker huyo wa ‘Number One’ kunyakua tuzo tatu kwenye tuzo za Channel O.
Diamond alikuwa ametajwa kwenye vipengele vinne. Vipengele hivyo ni pamoja na Most Gifted East Video, Most Gifted Afro Pop Video na Most Gifted Newcomer.
Kwenye tuzo hizo Diamond amefanikiwa kuwapiku wasanii nguli wa Afrika wakiwemo Iyanya, Davido, Flavour, Mafikizolo na Sauti Sol.
Ushindi huo umepokelewa kwa furaha kubwa na Watanzania wakiwemo wasanii wenzake.
“TANZANIA STAND UP! HE DID IT! @diamondplatnumz,” ameandika Davido.
“@diamondplatnumz wow congrats bro 3rd award already!! #cocobaby,” ameandika msanii wa Nigeria, Waje.
Naye Jokate Mwegelo aliyewahi kuwa mpenzi wake ameandika:
“Tanzania kwanza. Hongera sana @diamondplatnumz ….. Una vitu vyako vingi vya sijui project hiki an kile lakini kwenye ukweli naongea na siku zote mimi nakubali wewe una 1. Jitihada 2. Vision/Muono wa mbali 3. Kipaji ….. From Tandale to the World. You are a true inspiration. Watoto wengi sasa hivi wataamini wanaweza kufanikiwa kwasababu ya njia ulioweza kuionyesha wewe kwenye kazi zako. Keep on shining bruh. Tanzania tuko nyuma yako wewe na nyuma ya wale wote wenye vipaji na jitihada. It’s time Tanzania tukatoa vipaji zaidi na zaidi tukaweka team za ushabiki ambazo hazijengi pembeni na kujenga umoja utakaotuwezesha ku-take over Afrika na dunia nzima. Tanzania tunaweza. Haya usiku mwema. ”
Hitmaker wa Doc Shebeleza, Casper Nyovest naye amenyakua tuzo tatu, Most Gifted South Video, Most Gifted Male Video Doc na tuzo kubwa ya usiku huo, Most Gifted Video of the Year.
Hii ni orodha nzima ya washindi:
Most Gifted Video of the Year
Doc Shebeleza – Casper Nyovest
Most Gifted Male Video
Doc Shebeleza – Casper Nyovest
Most Gifted Female Video
Eminado – Tiwa Savage
Most Gifted Afro Pop Video
Number One – Diamond Platnumz
Most Gifted South Video
Doc Shebeleza – Casper Nyovest
Most Gifted East Video
Diamond
Most Gifted West Video
‘Turn Up’ – Olamide
Most Gifted duo/group/featuring
Pull Over – KCEE f/ Wizkid
Most Gifted Kwaito
Uhuru ft Oskido & Professor
Most Gifted RnB Video
‘Crazy But Amazing’ – Donald
Most Gifted Hip hop Video
Congratulate – AKA
Most Gifted Dance Video
Ngoku – Busiswa
Most Gifted Newcomer
Diamond Platnumz
Most Gifted Ragga Dancehall
Buffalo Souljah
[Continue Reading]

Monday, October 27, 2014

Ndoa ya Lady Jay Dee Sasa Basi Huu Ndio uthibitisho Kamili

Huku wakiendelea kugoma kuwa wameachana siri ya ndani ambayo inazidi kufumuka kwa mastaa wawili ambao wemetengana kinyumba ambao ni mwanamuziki Judith Wambura’Lady Jay Dee’na mtandazaji kiwango Gardner G Habash.
Taarifa za hivi zinaeleza kuwa Jaydee ameanza kumfuta Gardner kwenye urithi wa mali mbalimbali ili baadae wasije kuleteana shida kwenye mgao.

Chanzo cha ndani kinasema kuwa tayari Jaydee ameshauza nyumba moja huko kimara na ula mgahawa wa Nyumbani Lounge ambao aliutangaza kuufunga sasa anaufungua kwa jina la Mog Bar& Reutsaurant
“Kiukweli ni kwamba hawa jamaawameachana rasmi ila hawataki hili lijulikane kwa upande wa Lady Jaydee ameanza kulihakiki mali zote walizokuwa wakishea na Gadner kwa ajili ya kuzipa umiliki wake,tayari nyumba moja wameshauza na sasa amekodi upya ule mgahawa wa Nyumbani Lounge na utaanza kazi rasmi” chanzo hicho.
na kwa upande mwingine ladyjaydee amemtimua kazi rasmi Gadner kama meneja wake na sasa kazi zote zinazimamiwa na Rapa Wakazi
Credit : Udaku Specially
[Continue Reading]

Saturday, October 25, 2014

Breaking News – SITTI ABBAS MTEMVU AAMUA KUJIVUA TAJI LA MISS TANZANIA

Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zubeir Mtemvu.
Baada ya watu kuja na Ushahidi mbalimbali juu ya umri wake Sitti Mtemvu kupitia page yake ya facebook ameandika. 

[Continue Reading]

BAADA YA KUACHWA JAMAA ASAMBAZA PICHA ZA UCHI ZA DEMU MTANDAONI....Usisome habari hii kama una umri chini ya miaka 18

Mapenzi matamu pale yanapoanza na machungu pale mnapotengana,binti amejikuta katika wakati mgumu baada ya mpenzi wake kusambaza picha zake za U*CH*I kwenye mitandao ya kijamii baada ya binti kumtosa kidume na kuamia kwa kidume mwingine
ANGALIZO PICHA NI CHAFU SANA KAMA WEWE NI MTOTO TAFADHALI USIBOFYE PICHA HAPO CHINI HII NI KWA WAKUBWA TU
[Continue Reading]

Friday, October 24, 2014

MISS TANZANIA 2014 KUTUPWA JELA MIAKA MITATU ANGALIA HAPA

sitti 
Kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Vizazi na Vifo (sura ya 108) toleo la mwaka 2002, ni kosa la jinai kutoa taarifa za uongo kwa Msajili, na pia kosa la jinai kughushi. 
Alisema kwa sasa suala la Sitti limepelekwa kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo (Philip Saliboko) na mara baada ya kukamilika taarifa zake zitatolewa hadharani ili jamii ifahamu ukweli. 
“Huo mkanganyiko tumeshaupokea na tunaufanyia kazi, tutafanya kazi hii kwa kuzingatia na kufuata sheria na miongozo,” Kimaro alisema. “Rita imebaini kuwapo na udanganyifu wa aina hiyo ambao unafanywa na waombaji kwa kutuma maombi mapya baada ya kutakiwa kupeleka vyeti ili wapate ajira, kujiunga na vyuo au kusafiri nje ya nchi.

[Continue Reading]

MAMA KANUMBA: AFUNGUKA KUHUSU WEMA

Stori: MAYASA MARIWATA MAMA wa aliyekuwa nguli wa sinema za Kibongo, Steven Kanumba, Flora Mtegoa amempa darasa la kuzaa haraka mwigizaji Wema Sepetu na mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Msanii wa filamu Bongo Wema Sepetu.
Mama Kanumba alifunguka hayo hivi karibuni alipokuwa akipiga stori na mwanahabari wetu ambapo alipotakiwa kutoa ushauri juu ya penzi la Wema aliyewahi kuwa mpenzi wa mwanaye, mama huyo alisema azae haraka kwani umri haumsubiri.

“Kanumba hakuwahi kunitambulisha mwanamke yeyote zaidi ya Wema na aliapa kumuoa, akaniambia hawezi kuniletea mwanamke mwingine, nimshauri Wema azae na bebi wake kwani mtoto ni faraja kwake,” alisema mama Kanumba
[Continue Reading]

Wednesday, August 6, 2014

YOU HEARD: PENZI LA SHILOLE NA NUH MZIWANDA LAVUNJIKA..VIPI KUHUSU TATOO ALIYOJICHORA NUH ? CHECK HAPA


Siku ya jana haikua nzuri kwa Shilole na Nuh Mziwanda 

baada ya kugomabana sana hadi Nuh Mziwanda akaamua 

kuchukua vitu vyake na kuhama Kwa Shilole, Gazeti la 

Makorokocho imezipata taarifa hizi za motomoto kupitia 

kwa mtu 

aliyekuepo eneo la tukio aliyedai kuwa yeye alishangaa 

kuskia mikikimikiki ndani ya Harrier na baadae milango ya 

gari ikafunguliwa wakatokeza wasanii wawili wa bongo flava 

ambao ni Shilole na Nuh Mziwanda na walikua 

wakirushiana maneno ghafla wakatokeza watu 

wengine wakiongozwa na Msanii Chege 

Chigunda wakaamulizia ugomvi huo bila Mafanikio 

kwani Nuh Mziwanda alikua anamuambia Shilole

amrudishie simu yake lakini Shishi alishindwa kufannya 

hivyo kwa madai eti ufunguo upo nyumbani, Kweli? wakati 

dakika chache zilizopita walikua ndani ya Gari.

Nilipomtafuta Nuh Mziwanda hakutaka kubisha na akatiririka 

A to Z ya sakata hilo, Nuh Mziwanda: Jana Usiku tulialikwa 

Chakula Usiku kwa Producer Dibanjo, mitaa ya 

Mango Garden Kinondoni, mimi na Shilole tulipofika 

pale tukamkuta mwenyeji wetu pamoja na wasanii wengine 

Chege, Julio, Dully Sykes na wengine, ikafika muda nikawa 

sijiskii vizuri nikamuomba Shishi funguo ya gari ili 

nikapumzike kwenye gari, kufika kule nikazikuta simu za 

Shilole zikiwa na missed call nyingi pamoja na msg, 

nikazikagua na kukuta msg ya mwanaume akimwambia 

Shilole "Nimeingia Dar" .... ikabidi nimuite Shilole 

na kumkaripia sana Shishi akajitetea kuwa yule si bwana 

wake, Nikamwambia sawa mpigie niskie maongezi yenu, 

lakini Shishi alipompigia sikuelewa maongezi ndo 

nikamzaba kibao cha nguvu na Shishi akajibu mapigo kwa 

kuning'ata mwilini pamoja na kidole changu 

kimevimba mpaka wakati huu, watu wakajaa eneo la 

tukio hadi kina Chege wakafika na kuanza kuamulizia

kupigana lakini mwisho wa siku Shilole alikua amenipokonya 

simu yangu nilipomuomba akakataa kuirudisha na kuondoka  eneo la tukio,

Ikabidi na mimi nisepe kwenda Nyumbani kwa Shilole 

ambako nilikua naishi nae ila nia yangu ilikua ni kwenda 

kuchukua vitu vyangu ili nihame nyumba ile, njiani karibu 

nafika nikakutana na vibaka wakaniibia mpaka viatu, 

nikaendelea na safari lakini nilipofika pale kumbe Shishi 

alikua amempigia simu Dada wa Kazi asinifungulie mlango, 

ikabidi nikae hapo nje weeee mida mida Shilole akafika na 

kupitiliza ndani akajifungia mimi nikiwa nje, asubuhi 

wakajisahau na kuacha mlango wazi ndipo nilipopata 

upenyo nikaingia na kuchukua laptop, guiter pamoja na 

nguo vyote vyangu na kumwachia nyumba yake.

WEWE MDAU UNASEMAJE KUHUSU ILI ? JE ILE TATOO 

ALIYOJICHORA NUH MZIWANDA YENYE JINA LA 

SHILOLE ATAIFANYAJE ITOKE MWILINI MWAKE ?
[Continue Reading]

Friday, July 11, 2014

JE WAJUA ROSE NDAUKA AMKIMBIA MUMEWE, KISA MFUNGO

Staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka hivi karibuni aliamua kumkimbia mumewe Malick Bandawe, kisa mfungo wa Ramadhani ambapo sasa anaishi Kigogo na mama yake mzazi.
Staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka katika pozi.
Akipiga stori na Ijumaa, Rose alisema amelazimika kwenda nyumbani kwao ili kumpisha mumewe atimize nguzo hiyo ya Uislam bila kipingamizi kutokana na kutokufunga ndoa.
Rose Ndauka akiwa na mumewe, Malick Bandawe 
“Mimi sifungi hivyo nimeona pia ni jambo la busara kumpa nafasi mwenzangu kwa ajili ya kufanya ibada hiyo, mwezi ukiisha nitarudi na maisha yetu yataendelea kama kawaida,” alisema Rose ambaye awali alikuwa akiishi na mumewe huyo Tandale jijini Dar.
[Continue Reading]

Thursday, July 10, 2014

BABA ASEMA....: MAMA KANUMBA ‘PLIZ’ ACHA NJAA

BABA wa aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Bongo, marehemuSteven Kanumba, Charles Kanumba ameibuka na kumtaka mama Kanumba, Flora Mtegoa kuacha tabia ya kuombaomba michango mbalimbali.
Baba wa aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba.

Akipiga stori na paparazi wetu, Baba Kanumba alisema anashangazwa na tabia ya mama Kanumba kuombaomba ambapo hivi karibuni alimuona mjini Shinyanga ambako alikuwa akiomba rambirambi kwenye kumbi za starehe.
“Namshangaa mama Kanumba ni njaa gani hiyo, naomba aache kudhalilisha ukoo wa Kanumba kwani anatumia jina hilo kuombaomba, anahangaika bila sababu za msingi wakati sisi tuko vizuri,” alisema Baba Kanumba.

Mama Kanumba, Flora Mtegoa.
Akijibu tuhuma hizo, mama Kanumba alisema kama ana malalamiko yoyote aende mahakamani maana yeye si mume wake. “Aache kunifuatafuata kwani mimi si mkewe na Shinyanga nilialikwa kwenye Miss Shinyanga siyo kwamba nilijiendea tu,” alisema
[Continue Reading]

Tuesday, July 8, 2014

UMEYAONA MAJINA 403 YA WATANZANIA WALIFUNGWA NJE KWA MAKOSA KUUZA UNGA HAYA HAPA

Paparazi limeyanasa majina 403 ya Watanzania waliokamatwa, kufungwa au kushikiliwa katika magereza mbalimbali duniani kwa makosa ya madawa ya kulevya ‘unga’.

Baadhi ya watuhumuiwa wa kiume waliokamatwa kwa makosa ya kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya ‘unga’.

Hivi karibuni, serikali ilikiri kukamatwa kwa Wabongo hao nje ya nchi na kusema baadhi yao wanasubiri kunyongwa baada ya kupatikana na hatia. Hata hivyo, serikali ilificha majina ya watu hao.

Ifuatayo ni orodha ya majina hayo na maeneo wanayotoka nchini Tanzania. Kwenye mabano ni hukumu zao.

Abdallah Ally Rashid Mbonde Fredue, Dar (miaka 15 jela), Mzia David Michael, Dar (22), Rashid Mzonge, Magomeni, Dar (maisha), Salum Jumbe Pigigi (maisha), Ramadhan Iddi Juma, Kinondoni, Dar (7), Saleh Happy Hambona, Dar (18), Michael Dalasi Taraja, Temeke, Dar (19) na Juma Omar Mgeni (kunyongwa).

Wengine ni Masumbuko Salum Hassan, Dar (kunyongwa), Luka Joseph Urio, Dar (maisha), Masome Frorian Anthony, Dar (maisha), Salum Mohammed Kitupura, Dar (kunyongwa), Begge Hemed Ahmed, Tanga (15) na Mwanjati James Simon, Dar (maisha).

Wengine ni Mohammed Musa Mohammed, Dar (maisha), Omalla Donald Nyowino, Dar (15), Yahya Ally Seif, Kinondoni, Dar (maisha), Chande Mohammed Chande, Kinondoni, Dar (maisha), John James Amandus, Kinondoni, Dar (kunyongwa), Bantulaki Isihaka Ally, Tanga (kunyongwa), Zungiza Mohamed Ally, Dar (kunyongwa), Rashid Bakari Mzonge, Kimara Suka, Dar (maisha), Mende Katija Mikidadi, Ilala, Dar (maisha), Shame Shame Udai, Dar (maisha) na Mlenzi Mangala Hamisi, Dar (maisha).

Baadhi ya watuhumuiwa wa kike waliokamatwa kwa makosa ya kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya ‘unga’. Farida Sarboko Makarani, Zanzibar (kunyongwa), Adam Hariri Mohammed, Magomeni, Dar (18), Said Mfaume Said, hajatajwa wa wapi (kunyongwa), Mohammed Bakari Mkemi, haijatajwa wa wapi (kunyongwa), Mariam Ramadhan Mahimbo, hajatajwa wa wapi (kunyongwa), Julieth Jonathan Jaspher, haikusemwa anakotoka (kunyongwa), Halifa Matumla Ally, haijaandikwa atokako (kunyongwa), Rajabu Salum Mwanyenza, haijaandikwa atokako (kunyongwa), Ismail Mohammed Rajabu Mapusa, Magomeni Dar (maisha) na Hamisi Kombo Ally (kunyongwa).

Waliopo mbaroni ambao pia hawajaandikwa watokako ni: Sephu Abdulrahman, Alfredy Thomas Singini, Lawrence Mbogoni Oni, Mohammed Ibrahimu Kilima, Wilfred Casmir Mushi, Shakira Ahmed Mumba, Jackline Benedict, Rajabu Rashidi Mshare, John Peter Martin, Abdallah Mwalimu Mbaruk, Rashid Mzee Mrisho, Juma Ismail Nayopa, Tsakiris Costa Achelis na Faith Michael Kabambe.

Wengine waliohukumiwa ni Bakari Badi Omari Mneko, Sinza, Dar (17), Masomi Thomas Joseph, Dar (17), Abdallah Iddi Ally, Tabata, Dar (17), Kondo Ally Mohammed (20), Mohammed Abubakar Nazzir (24), Abdallah Anwar Abasi (24), Makuti Al- Jaribu Hassan, Kilwa, Lindi (25), Abdallah Iddi Athuman (24), Mnyamani Hamad Ally, Tanga (22), Mtalu Rajabu Ally Rajabu, Kariakoo, Dar (17) na Shughuli Kibaya Bakari, Tanga (8).

Wengine ni Mfaume Omar Ng’anzi Msuya, Kariakoo, Dar (21), Steven Robert Onay (9), Omar Juma Mang’enge (8), Steven Simon Kanul, Dar (8), Iddi Haji Fumo, Unguja (9) na Seleman Hamisi, Unguja (8).

Pia wapo Athuman Hassan Nash, Magomeni, Dar (8), Seleman Hussein Msimbe (8), Abdallah Farid Twalib, Dar (17), Salim Ally Amani, haikutajwa anakotoka (22), Calist Wilson Mosha, Arusha (18) na Saleh Abdul Omar, Kigogo, Dar (21).

Wengine ni Bugingo Sweetbert Rwezaura, Kijitonyama, Dar (21), Mohammed Omari Ally, Zanzibar (19), Sayula Rashid Paul, hajatajwa atokako (16), Koshuma Geofrey Gabriel, Kijitonyama, Dar (30) na Salim Mrisho Hussein, Tanga (21).

Orodha inaendelea kama ifuatavyo: Riziki Riziki Hamduni, Kinondoni, Dar (19), Bashir Rajabu Kafune, Magomeni, Dar (19), Kharim Mohammed Omar, Ilala, Dar (19), Abubakar Abdul Ligalwike, Kinondoni, Dar (8).

Wengine waliofungwa na miaka yao katika mabano ni Pendo Ernest Kessy, Ilala, Dar (9), Anna Kiula, Kijitonyama, Dar (9), Nuru Shebe Maftah, Mwananyamala, Dar (9), Fatma Rashid, Dar (9) na Naima Abdulhafidh Rashid, Mwananyamala, Dar (9).

Pia wapo Mariam Madaresa, Arusha na Dar (9), Mohammed Omar Ally, Wete, Zanzibar (19), Faidhi Mohammed Abdallah, Kijitonyama, Dar (14), Mohammed Ijumaa Rashid, Mbezi Beach, Dar (10), Omari Musa Abdallah, Tanga (10), Zahra Ayubu Mwila, Korogwe na Kibaha (25) na Shamsa Gulum Shambe, Magomeni Mwembechai, Dar (16).

Wengine waliopo mbaroni ni Jeniffer Kessy, Mwananyamala, Dar, Shadia Issa, Mbezi Beach, Dar, Rosemary Asakwe Kionaumela, Mapipa, Dar na Samir Sandra Khalid.

Orodha ya waliohukumiwa inaendelea: Tatiana Bakari Chambo, Temeke, Dar (11), Ramadhan Maneno Mtumwa, Kijitonyama, Dar (14), Yusuf Herold John, Magomeni (18), Hassan Hiza Sebudu, Tanga (22), Halfa Abdallah Ng’anga, Ilala, Dar (19) na Nelson Anthony Dhinner, Kigogo, Dar (14).

Wengine waliohukumiwa ni Awadh Salehe Awadh, Kinondoni, Dar (24), Hasim Paul Syula, Mapipa, Dar (16), Fussy Abdu Mussa, haijatajwa anakotokea (17), Mtwanzi Carlos Adam, haijatwaja anakotoka (17) na Yusuf Abbas Kilima, Dar (5).

Wafuatao wametiwa mbaroni; Salum Mhibu Mkwawira, Tunduma, Mbeya, Juma Musa Juma wa Zanzibar, Nassor Mohammed Ayub wa Tanga, Jimmy Joseph Kivelege wa Dar, Kilugage Joram Masembo wa Kahama, Shinyanga, Manengelo Abdurahman wa Dar na Hamud Ali Mohammed (mji haukutajwa).

Wengine ni Eric Charles Mkude wa Tanga, Makame Khatibu Ali wa Kiembesamaki, Zanzibar, Abdulwahid Hamisi Mashauzi wa Singida, Said Ally Makame wa Zanzibar, Peter George Gyellah wa Tegeta, Dar, Said Abdallah Mzee wa Dar na Yusuf Chombo Khalid wa Dar.

Wafuatao wamehukumiwa na miaka yao kwenye mabano; Salehe Mohammed Aboubakar, Tanga (20), Abdul Omar Salehe, Dar (14), Omari Hussein Ally, Tanga (14), Kaliro Samson Majani Busagaga, Tarime, Mara (9), Mohammed Salum Mbaraka, Moshi, Kilimanjaro (9), Zuberi Musa Zuberi, Zanzibar na Dar (9), Adam Athumani Udindo (alikataa kutaja anakotoka, 14).

Wafuatao pia wapo mahabusu katika nchui mbalimbali, kesi zinaendelea; Frank Thomas Frank (Moshi), Nasra Hassani Masogoa (Dar), Nice Saidi Mbwana (Tanga na Dar), Josephine Raymond Malibanga (hakutaja atokako), Sara Yuga Mtinda (Singida), Amina Khamisi Bwanga (hakutaja atokako), Flora Frederick Siyame (Dar) na Zawadi Aloyce Henjewele (Songea).

Wengine ni Upendo Eric Shayo wa Moshi, Mariam Haruna Feruzi (Dar), Yusta Riwa (Moshi Kilimanjaro), Watende Sudi Kiwamba (Tabora), Elizabeth Yoram Kwambaza (Korogwe, Tanga), Mariam Shabibi (Dar) na Zahoro Mohammed Nassoro (Tanga).

Wengine waliokamatwa na wako mahabusu ni Rashid Nassoro Maumba (Mpanda), Mohamed Said Mrisho (Tanga), Suleiman Said Mpetula (Dar), Shaban Salum Mnyimani (Dar), Abood Yasser Ali (Tanga), Juma Shabani Ngoma (Tanga), Juma Akida Yusufu (Tanga) na Miraji Yusufu Semahimbo (Tanga).

Wengine ni James Christopher Lukio (Tanga na Dar), Rabin Issa Mbaba (Mafia), Abdallah Rajabu Dole (Dar), James Sakaya Henry (Dar), Bakari Kheri Nassoro (Dar), Faraji Juma Lota (Dar), Gervas Anselm Muganda Matura (Musoma), Rawe Waikama Magarya (Tarime) na Abdulraheem Sadiki Mohamed (Dar).

Wafuatao wamehukumiwa na miaka yao kwenye mabano ila miji waliyotoka Bongo haikutajwa; Rashid Habib Muhsin (9), Abdallah Saidi (16), Hiridi Mamdadi Issa (12), Juma Mohammed Mapande (16), Mwatadi Kulwa Hamisi (16), Hamisi Abdallah Mohammed (9), Erick John Ibrahim (16) na Abdallah Farid Salum (9).

Thuweni Hamadi Suleiman, Kileo Walter Exaudy na Jacqueline Clifford Fitzpatricque (Jack Patrick) hawa bado hawajahukumiwa.

IDADI YA NCHI

Katika orodha hiyo, China wapo Wabongo 65, Brazil 108, Kenya 34, Hong Kong 118, Pakistan 16, Falme za Kiarabu 12, Japan 7, Morihsaz 6, Uingereza 5, Malawi 5, Uganda 4, Oman 3, Uswisi 2, Italia 2, Marekani 2, Argentina 2, Uturuki 1, Ureno 1, Botswana 5, Chile 1, Afrika Kusini 3 na Msumbiji 1.

paparazi aliongea na Kaimu Kamishna wa Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya, Aida Tesha (pichani) kuhusu kukamatwa kwa watu hao ambapo alikiri na kusema kuwa serikali inaendelea kufuatilia takwimu za Watanzania wengine ambao wamekamatwa nje ya nchi.
[Continue Reading]
Powered By Blogger · Designed By Seo Blogger Templates