Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

Wednesday, February 18, 2015

RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAPYA 27


*Atengua uteuzi wa Ma-DC 12, awabadilisha vituo 64, awabakiza 42 kwenye vituo vyao vya zamani

RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Wakuu wapya 27, kuwahamisha vituo vya kazi 64 na wengine 42 amewabakisha kwenye vituo vyao vya kazi vya zamani.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI leo mchana (Jumatano, Februari 18, 2015) Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo zilitokana na wakuu wa wilaya watatu kufariki dunia; kupandishwa cheo wakuu wa wilaya watano, kupangiwa majukumu mengine wakuu wa wilaya saba na kutenguliwa kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya 12.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema, Rais Kikwete amewabadilisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 64 na kuwabakiza kwenye vituo vyao vya zamani wakuu wa wilaya 42.

Wakuu wa Wilaya wapya 27 walioteuliwa ni Mariam Ramadhani Mtima anayeenda Ruangwa; Dk. Jasmine B. Tiisike anayeenda Mpwapwa; Pololeti Mgema (Nachingwea); Fadhili Nkurlu anayeenda Misenyi; Felix Jackson Lyaniva anayeenda Rorya na Fredrick Wilfred Mwakalebela anayeenda wilayaya Wanging’ombe.

Wengine na vituo vyao kwenye mabano ni Zainab Rajab Mbussi (Rungwe); Francis K. Mwonga (Bahi); Kanali Kimiang’ombe Samwel Nzoka (Kiteto), Husna Rajab Msangi (Handeni), Emmanuel J. Uhaula (Tandahimba); Mboni Mhita (Mufindi); Hashim S. Mgandilwa (Ngorongoro); Mariam M. Juma (Lushoto); Thea Medard Ntara (Kyela); Ahmad H. Nammohe (Mbozi); Shaban Kissu (Kondoa) na Stephen Zelothe (Musoma).

Wengine ni Pili Moshi (Kwimba); Mahmoud A. Kambona (Simanjiro); Glorius B. Luoga (Tarime); Zainab R. Telack (Sengerema); Bernard Nduta (Masasi); Zuhura Mustafa Ally (Uyui); Paulo Makonda (Kinondoni); Mwajuma Nyiruka (Misungwi) na na Maftah Ally Mohamed (Serengeti).

Wakuu wa Wilaya saba ambao uteuzi wao umetenguliwa lakini watapangiwa kazi nyingine ni Brig. Jenerali Cosmas Kayombo aliyekuwa Simanjiro; Kanali Ngemela E. Lubinga (aliyekuwa Mlele); Juma S. Madaha (aliyekuwa Ludewa); Mercy E. Silla (aliyekuwa Mkuranga); Ahmed R. Kipozi (aliyekuwa Bagamoyo); Mrisho Gambo (aliyekuwa Korogwe) na Elinas A. Pallangyo (aliyekuwa Rombo).

Waziri Mkuu pia aliwataja Wakuu wa Wilaya 12 ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na sababu za umri, kiafya na kuimarisha utendaji Serikaini na wilaya zao kwenye mabano kuwa ni James K. Ole Millya (Longido); Elias Wawa Lali (Ngorongoro); Alfred Ernest Msovella (Kongwa); Danhi Beatus Makanga (Kasulu); Fatma Losindilo Kimario (Kisarawe); Elibariki E. Kingu (Igunga); Dk. Leticia Moses Warioba (Iringa); Evarista N. Kalalu (Mufindi); Abihudi M. Saideya (Momba); Martha J. Umbulla (Kiteto); Khalid J. Mandia (Babati) na Elias Goroi (Rorya).


(mwisho)


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMATANO, FEBRUARI 18, 201
[Continue Reading]

Monday, July 7, 2014

KIONGOZI WA CHADEMA MKOANI KIGOMA ASHAMBULIWA NA WATU WASIOJULIKANA

Maelezo ya picha; Makamu mwenyekiti Uenezi CHADEMA kanda ya Magharibi Deogratius Liyunga akiwa amelazwa katika Hospital ya Mkoa wa Kigoma(Maweni)baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana(Picha na Editha Karlo).
Na Editha Karlo, Kigoma.
WATU wasiojulikana wamemvamia na kumpiga pamoja na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili kwa kutumia vitu vyenye ncha kali Makamu Mwenyekiti wa uenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kanda ya Magaharibi,Deogratius Liyunga na kupelekea kulazwa katika Hospita ya Mkoa wa Kigoma (Maweni)
[Continue Reading]

Tuesday, May 6, 2014

Boko Haram kuwauza wasichana waliotekwa

Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau
Kundi la wapiganaji wa kiislamu nchini Nigeria la Boko Haram limesema linapanga kuwauza wasichana zaidi ya miambili ambao liliwateka nyara wiki tatu zilizopita
Hii ni baada ya kundi hilo hatimaye kukiri ndilo lililowateka wasichana hao baada ya kimya cha wiki tatu tangu kutekwa nyara kwao.
Kiongozi wa kundi hilo, Abubakar Shekau alituma kanda ya video ambapo alikiri kwa mara ya kwanza kuwa kundi hilo ndilo liliwateka nyara wasichana hoa.
Wasichana hao walitekwa kutoka shule moja iliyo kaskazini mashariki mwa nchi walipokuwa wajinadaa kwa mitihani yao.
Wakati huo huo mwanamke ambaye ni kiongozi wa maandamano ya kushinikiza serikali kuharakisha juhudi zake za kuwaokoa wasichana hao, nchini humo Naomi Mutah aliyekuwa amezuiliwa na polisi kwa amri ya mke wa rais wa nchi hiyo Patience Jonathan ameachiwa huru.
Kumekuwa na shinikizo kwa serikali ya nchi hiyo kwamba haijafanya juhudi kubwa kuwaokoa wasichana hao.
Akizungumza kwa mara ya kwanza kuhusu tukio hilo rais wa Nigeria Goodluk Jonathan amesema kuwa atafanya awezalo kuwakoa wasichana hao.
Takriban watu 1500 wameuawa na kundi hilo mwaka huu likisema kuwa linapigana dhidi ya kile linachosema ni elimu ya kimagharabi.
[Continue Reading]

Sunday, March 16, 2014

RIDHIWANI KIKWETE AANZA KAZI YA KUZISAKA KURA JIMBO LA CHALINZE

Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake kwa wakazi wa Kijiji cha Miono,Wilayani Bagamoyo leo Machi 15,2014,ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Mikutano ya Kampeni zake za Uchaguzi huo mdogo wa Jimbo la Chalinze unaotarajiwa kufanyika Aprili 6,2014.Picha zote na Othman Michuzi.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete pamoja na Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Steven Kazidi wakiwa na Mama wa Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Chalinze (aliefariki Dunia),Marehemu Said Bwanamdogo wakati walipofika kumjulia hali nyumbani kwake Kijijini Miono,Bagamoyo leo Machi 15,2014.
Meneja wa Kampeni katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa Kumpigia debe Mgombea Ubunge katika Jimbo hilo,Ridhiwani Jakaya Kikwete (hayupo pichani),uliofanyika leo Machi 15,2014 kwenye Kijiji cha Kimange.
"Kinamama huko,inamaana hakuna vigelegeleeeee .....???" hivyo ndivyo alivyokuwa akiuliza Diwani wa Kata ya Kimange,Hussein Hading'oka (pichani) wakati alipokuwa akimwaga sifa kede kede kwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi wa Kijiji cha Kimange,Kata ya Kimange,Wilayani Bagamoyo leo Machi 15,2014, wakati akiwasili kwa ajili ya Mkutano wa Kampeni zake za Uchaguzi huo mdogo unaotarajiwa kufanyika Aprili 6,2014.Picha zote na Othman Michuzi.
Meneja wa Kampeni katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi (kulia) akizungumza jambo na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete kabla ya kumpatia kipaza sauti ili aweze kuzungumza na wanakijiji wa Kimange.

BOFYA READ MORE KWA PICHA ZAIDI

Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kimange,Kata ya Kimange Wilayani Bagamoyo leo Machi 15,2014,wakati wa Mkutano wa Kampeni zake za Uchaguzi huo mdogo wa Jimbo hilo unaotarajiwa kufanyika Aprili 6,2014.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akijumuika pamoja na wanakijiji wa Miono,Wilayani Bagamoyo kwenye dua maalum ya kumuomba Mwenyezi Mungu ajaalie mafanikio mema katika kumuongoza Mgombea Ubunge huyo kwenye mwendelezo wa Kampeni zake.
Dua ikiendelea.......
wakiwa wamesimama kwa dakika moja kumkumbuka aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Marehemu Said Bwanamdogo.
"Shkamoo Bibi....."
Ridhiwani akiendelea kumwaga sera zake.

Wananchi wakifatilia Hotuba ya Mgombea wao kwa Umakini mkubwa.
Wadau wa Kijiji cha Kimange wakichukua taswira ya Mgombea wao kupitia simu zao za mikononi.
"Mtoto Mzuri naomba Kofiaaaaa"
Wananchi wakimsikiliza Mgombea wako kwa makini.
Nyundo na Jembe ndio mpango mzimaaaa......
"Kijana wetu wewe ndie tunaekutaka,na amini utashinda kwa kishindo" ndivyo alivyosikika mama huyu akimwambia Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete.
Mkutano kwa siku ya leo ulimalizikia katika Kijiji cha Mbwewe,Pichani ni Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze akipita katikati ya vijana wa chipukizi wakati akiwasili kwenye Kijiji hicho.
Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kulia) akifurahia baada ya kupewa maneno ya kuvutia kutoka kwa vijana wa chipukizi.


[Continue Reading]

Friday, March 14, 2014

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YATOA UFAFANUZI KUHUSU DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA KALENGA


Pichani Kati ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Mh.Jaji Mstaafu Damian Lubuva akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema leo mchana,kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ya Hill Top Hotel,mjini Iringa kuhusiana na ufafanuzi wa Daftari la Kududumu la Wapiga Kura litakalotumika katika Uchaguzi wa Ubunge jimbo la Kalenga,unaotarajiwa kufanyika machi 16 mwaka huu.Jaji Lubuva amebainisha kuwa Tume haijafanya Uboreshaji kwa maana ya kuandikisha Wapiga kura wapya ambao hawakuwa wamejiandikisha kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010.

"Kilichofanyika Mwaka 2014 ni Uhakiki wa Daftari hilo ili kuwa sahihi zaidi na kuhakikisha kila aliyeandikishwa hapo awali na kupewa kadi ya kupigia kura anatumia haki yake ya kupiga kura,hii ni kuondoa malalamiko ya kushindwa kupiga kura kwa sababu ya kukosekana jina lake kwenye Daftari",amesema Jaji Lubuva.Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Mh.Julius Mallaba na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid.

Amesema kuwa kutokana na Uhakiki uliofanyika,ukweli ni kwamba taarifa za wapiga kura zilizohakikiwa zilikuwa 149 tu.Wapiga kura walioongezeka katika Daftari lililotumika katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 ni saba (7) tu na sio 600 kama ilivyotolewa taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya habari

 Baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Mh.Jaji Mstaafu Damian Lubuva akitoa ufafanuzi wa Daftari la Kududumu la Wapiga Kura litakalotumika katika Uchaguzi wa Ubunge jimbo la Kalenga,unaotarajiwa kufanyika machi 16 mwaka huu.Jaji Lubuvu amebainisha kuwa Tume haijafanya Uboreshaji kwa maana ya kuandikisha Wapiga kura wapya ambao hawakuwa wamejiandikisha kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010. credit;michuzi
[Continue Reading]

Tuesday, March 11, 2014

MTOTO WA RAISI JAKAYA KIKWETE RITHIWAN KUWANIA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE TAARIFA KAMILI IKO HAPA.

Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imemteua, Ridhiwani Kikwete, kuwa mgombea katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani, unaotarajiwa kufanyika Aprili 6, mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, uzinduzi wa kampeni za CCM utafanywa na Katibu Mkuu wa chama hicho Taifa, Abdulrahaman Kinana na kufungwa na Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein.
Alisema kampeni katika jimbo hilo zitaendeshwa na chama hicho ngazi husika na kuratibiwa na yeye mwenyewe Nnauye.
“Aidha kikao hicho cha Kamati Kuu, kilipokea taarifa ya maendeleo ya kampeni zinazoendelea huko Kalenga, huku ikisema imeridhika na mwenendo wa kampeni hizo, ambapo CCM inatarajia kupata ushindi,” alisema.
Katika uchaguzi wa kuwania nafasi hiyo ya ubunge Chalinze, Ridhiwani alishinda katika kura ya maoni kwa kupata kura 758, akifuatiwa na Shaban Madega kura 335, Athuman Maneno kura 206 na Changwa Mkwazu aliyepata kura 12.
Wakati huo huo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza rasmi mgombea wa ubunge katika Jimbo la Chalinze kuwa ni Mathayo Torongei.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkuu wa Operesheni ya Uchaguzi Chalinze wa chama hicho, John Mrema, alisema Torongei alishinda nafasi hiyo ya kuwania ubunge kwa tiketi ya chama hicho baada ya kuwamwaga wenzake watatu katika kura zilizopigwa na Kamati Kuu ya chama hicho juzi.
Alisema pamoja na ushindi huo wa kuthibitishwa na Kamati Kuu ya chama hicho, Torongei alishawamwaga wenzake hao katika kura ya maoni ya wanachama wa chama hicho, Jimbo la Chalinze kwa kupata kura 280 kati ya 478 ya kura zote zilizopigwa.
Wagombea wengine waliojitokeza katika uchaguzi huo ni pamoja na Francis Mgasa aliyepata kura 61, Frank Mzoo (23) na Mwenyekiti wa Jimbo la Chalinze wa chama hicho, Omary Mbambo aliyepata kura 84.
“Uteuzi wa mgombea huyu umefuata utaratibu wote za chama na Kamati Kuu imezingatia maoni na ushauri wa wanachama. Torongei ana historia nzuri na Chadema na tuna uhakika atashinda kwa kishindo Chalinze,” alisema Mrema.
Alisema chama hicho kimeamua kusimamisha mgombea katika jimbo hilo, ili kusaidia wananchi wa Chalinze kutatuliwa matatizo yao yaliyodumu kwa muda mrefu.
Kwa upande wake, Torongei aliwashukuru wanachama wa chama hicho Jimbo la Chalinze, kwa kumuamini na kumchagua na kuwaahidi kuwa endapo atashinda nafasi hiyo, atamaliza kero zao, hasa tatizo la migogoro ya wakulima na wafugaji.
“Mimi nimezaliwa na kukulia Chalinze, ni mtoto wa Chalinze na mtoto wa mkulima. Ninaifahamu vilivyo Chalinze kuliko mtu yeyote,” alijitapa.
Kwa upande wake, Chama cha Wananchi-CUF kimemteua Fabian Leonard kuwa mgombea wake wa ubunge Jimbo la Chalinze.
Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Abdul Kambaya alitangaza hayo, makao makuu ya chama, Buguruni Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Kambaya alitamba kuwa CUF inakwenda kuchukua jimbo hilo na kwamba Leonard analijua vema jimbo hilo, kwani alishawania ubunge katika jimbo hilo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2000, ambapo alipambana na mgombea ubunge wa CCM, ambaye wakati huo alikuwa Rais Jakaya Kikwete.
“Huyu Leonard ni mzaliwa wa Chalinze na anayajua matatizo ya wana Chalinze. Alisisitiza kuwa Leonard amejipanga vyema na ana uhakika atashinda.
Uchaguzi mdogo wa jimbo hilo la Chalinze, unatarajiwa kufanyika Aprili 6, mwaka huu.
Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), vyama vya siasa vinapaswa kuwasilisha majina ya wagombea wao kesho kwa ajili ya kuthibitisha uteuzi wao. Kampeni rasmi za uchaguzi huo, zitaanza kesho kutwa.
Uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Said Bwanamdogo kufariki dunia.
[Continue Reading]

Saturday, February 22, 2014

CHADEMA VIPANDE VYAENDELEA KUKATIKA,SASA KATIBU WILAYA ATIMULIWA

KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Mvomero, imedaiwa kumvua Uongozi Katibu wa Wilaya wa Chama hicho hicho wilayani humo, Mrisho Ramadhani, kwa madai ya kukisaliti Chama.

Habari toka ndani ya kikao cha siri kilichoketi Ofisi ya Wilaya zinadai, Kamati ilimvua ukatibu Mrisho kutokana na kufanya maamuzi ya kukiunganisha Chadema na Vyama vingine bila ridhaa ya Chama, na kumdharilisha Diwani wake, Luka Mwakambaya.

Akizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina Mtoa habari wetu alisema, Mrisho amebakiwa na Ukatibu Mwenezi wa Wilaya, amabapo suala lake limepelekwa kwenye Mkutano Mkuu akajadiliwe na kutolewa maamuzi.

“Baada ya Chadema kutangaza kufanya mkutano wa M4C–Opresheni ya Pamaoja Daiama (OPD) Kata ya Mtibwa 29.1.2014, Mrisho aliacha Sera za Chadema za kutatua kero za wakulima na wafanyakazi zilizofanywa na Mwakambaya na kuungana na wanaokwamisha OPD.

“Kama haitoshi, 29.1.2013, alimdharilisha Diwani wa Kata ya Mtibwa, Mwakambaya (Chadema) katika Mkutano hadhara, akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe, aliyetaka aelewe Kero za Mwekezaji wa Mtibwa aende nazo bungeni”.alisema mtoa habari.


Mkutano huo Mrisho alisema, ‘kutokana na kero za mwekezaji wa Mtibwa kukithiri akiwacheleweshea malipo Wakulima wa wadogo wa miwa na wafanyakazi, Chadema kimeungana na Vyama vingine kudai haki kwa maandamano baada ya Diwani Mwakambaya kushindwa, jambo ambalo halikuwa kweli na lilipingwa na wananchi, kwa sababu amekuwa akilala langoni mwa lango la mwekezaji na kulazimika kuwalipa.

Aidha baada ya Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mvomero Saimanga Kashikashi kutafutwa bila mafanikio, alimtafutwa Mwenyekiti wa Kanda ya Kati Msingi Chadema, Innocent Zawadi kutaka kujua suala hilo, naye alisema ngoja awasiliane na uongozi wa Wilaya ya Mvomero kupata habari sahihi.

Nafasi ya Katibu wa Wilaya ya Mvomero (Chadema) tangu uchaguzi ufanyike, imekuwa ikipyaya na kukaimishwa kwa mara pili sasa, ambapo baada ya kikao hicho jana imekaimishwa kwa, Rosemaary Kimune, huku wapenzi wa Chadema wakikitaka chama kutafuta mtu makini.

-williammalecela blog
[Continue Reading]

Wednesday, February 19, 2014

DU! KIGOGO WA CCM AFUNGUKA NA KUKIPONDA CHAMA CHAKE CCM BUNGENI LAIVU BILA CHENGA



‘’TULINYESHEWA mvua pamoja, tulipigwa na baridi tukiwa pamoja, kuna maeneo mengine tulipigwa mawe na hata kuzomewa tukiwa sote, tuliwakiwa na jua tukalala porini, leo hii Jakaya yuko Ikulu sisi bado tupo barabarani!!!
‘’ Nazungumza haya kwa uchungu mkubwa , tunatumika sisi mnapofanikiwa mnatusahau kama mafanikio yenu yametokana na sisi, CCM haiwezi kujivunia mafanikio yake bila kututaja sisi,tumekuwa ndiyo nembo ya chama hiki, tumeingia humu kukiwa giza totoro, hakukuwa na mshahara wala chochote wengine tulilazimishwa hata kuacha kazi kwa ajili ya hiki chama!!
‘’Mzee Kinana unakumbuka wakati ule unatufundisha kule jeshini kwmaba lazima tuwe wakweli, na mimi nasema ukweli uliopo ndani ya moyo wangu sikwepeshi maneno, jamani!! Eeh tukumbukeni hata angalu tunapostaafu, tustaafu vizuri, angalieni hawa wasanii wameingie leo katika chama, mnajua hii kwao ni gharama kubwa kazi zao za usanii zitakuwa katika mazingira magumu iwapo hamtawaenzi na kuwawekea mazingira mazuri.
‘’Ukweli ni kwamba kwa kuwa wamejionesha wao ni CCM sasa hivi kazi zao zitanunuliwa na wanaCCM tu, lakini tukumbuke kuwa CCM sio Watanzania wote, watajengewa chuki na uadui na kazi zao zitakuwa ngumu kuuzika!!
‘’Mwangalieni huyu kijana anaitwa Maro aliipigia kampeni sana CCM wakati ule wa uchaguzi mkuu leo hii yuko wapi anaishi katika mazingira magumu kwa kuwa alijiweka wazi, tuambieni CCM mmemfanyia nini kijana huyu? Ni baadhi ya maneno yaliyogusa hisia ya Kapteni John Komba alipoamua kutoa dukuduku lake wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na CCM kati ya waandishi wa habari na Wasanii kwenye ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya jana usiku.
Kapteni John Komba alienda mbali zaidi na kumueleza Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kwamba wao Bendi ya TOT imekuwa ikitumika kwa kampeni kwa miaka mingi bila mafanikio yoyote kwa wasanii wa bendi hiyo na kuwa tangu wakati wa Mzee Mwinyi, Mkapa na sasa Rais Jakaya Kikwete hakuna manufaa yoyote kwa wasanii hao ambao wamechangia kwa asilimia kubwa ushindi wa CCM.
Alisema yeye binafsi hana matatizo sana bali kinachomuuma ni mustakabali wa wasanii ambao ndio kwanza wanachipukia na wanategemea kipato chao kwa kazi za usanii na kuwa kuna jitihada za CCM kuangalia vyema wanaosaidia kukifikisha hapo chama hicho watazamwe kwa jicho la yakini.
Huku akishangiliwa na wasanii ilhali Katibu Mkuu wa CCM Kinana akiwa amejiinamia kwa tafakari juu ya maneno hayo yalaiyowagusa wasanii wengi waliohudhuria hafla hiyo, Kapteni Komba alichukua fursa hiyo pia kuwasemea waandishi wa Habari ambao nao wamekuwa wakitumika kwenye kampeni baadaye wanasahauliwa.
‘’Hata Waandishi wa Habari, wamefanya kazi kubwa sana kuwafikisha hapo mlipo lakini leo hii mko kwenye neema mnaweza kusema kuna jambo gani kubwa walionufaika nalo? Alihoji Kapteni Komba.
Naye Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye alisema kuwa kuna haja ya chama hicho kuangalia namna nyingine ya kuwajali wale wanaosaidia kukifikisha hapo CCM na kutolea mfano wakati wa makatibu wakuu waliopita kwa kuwataja majina akina marehemu Horace Kolimba,Philip Mangula, Yusuf Makamba,Wilson Mukama na sasa Kinana.
Alisema tangu alipoingia Kinana kumekuwa na mwanga kidogo wa mafanikio hivyo kwa kuwa anayo fursa ya kuzungumza na Mwenyekiti wa CCM Taifa (JK) amueleze kilio hicho na kuwa hiyo ndiyo hali na mazingira halisi inayowakumba watu wanaotumiwa kuisaidia CCM kwa kampeni na kuifikisha hapo ilipo.
Katika maadhimisho ya miaka 37 ya CCM wasanii wa Bongo Movie Single Mtambalike( Richie) JB,Irene Uwoya,Amanda, Omar Mrisho(SLIM),Haj Rajab,Banana Zorro, Haj Rajab na Wastara Juma walijiunga na chama hicho na kukabidhiwa kadi na Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete.



Mjumbe wa NEC na Mbunge wa Mbinga Kapteni John Komba katika moja ya vikao vya Bunge mjini Dodoma


Msanii wa Bongo Movie Banana Zorro akiwa katika uwanja wa Sokoine jana, Banana na wasanii wenzie walijiunga na CCM na kukabidhiwa kadi na Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete

Wastara Juma na JB pamoja na wasanii wenzie wa Bongo Movie wakiwa katika uwanja wa Sokoine ambako walikabidhiwa kadi na Rais Jakaya Kikwete.


[Continue Reading]
Powered By Blogger · Designed By Seo Blogger Templates