Pichani Kati ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Mh.Jaji Mstaafu Damian Lubuva akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema leo mchana,kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ya Hill Top Hotel,mjini Iringa kuhusiana na ufafanuzi wa Daftari la Kududumu la Wapiga Kura litakalotumika katika Uchaguzi wa Ubunge jimbo la Kalenga,unaotarajiwa kufanyika machi 16 mwaka huu.Jaji Lubuva amebainisha kuwa Tume haijafanya Uboreshaji kwa maana ya kuandikisha Wapiga kura wapya ambao hawakuwa wamejiandikisha kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010.
"Kilichofanyika Mwaka 2014 ni Uhakiki wa Daftari hilo ili kuwa sahihi zaidi na kuhakikisha kila aliyeandikishwa hapo awali na kupewa kadi ya kupigia kura anatumia haki yake ya kupiga kura,hii ni kuondoa malalamiko ya kushindwa kupiga kura kwa sababu ya kukosekana jina lake kwenye Daftari",amesema Jaji Lubuva.Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Mh.Julius Mallaba na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid.
Amesema kuwa kutokana na Uhakiki uliofanyika,ukweli ni kwamba taarifa za wapiga kura zilizohakikiwa zilikuwa 149 tu.Wapiga kura walioongezeka katika Daftari lililotumika katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 ni saba (7) tu na sio 600 kama ilivyotolewa taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya habari
Baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Mh.Jaji Mstaafu Damian Lubuva akitoa ufafanuzi wa Daftari la Kududumu la Wapiga Kura litakalotumika katika Uchaguzi wa Ubunge jimbo la Kalenga,unaotarajiwa kufanyika machi 16 mwaka huu.Jaji Lubuvu amebainisha kuwa Tume haijafanya Uboreshaji kwa maana ya kuandikisha Wapiga kura wapya ambao hawakuwa wamejiandikisha kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010. credit;michuzi
No comments: