Showing posts with label MATUKIO. Show all posts
Showing posts with label MATUKIO. Show all posts

Tuesday, March 31, 2015

Tamko la maaskofu na wachungaji wa kipentekoste juu ya kuugua ghafla kwa askofu Gwajima

TAMKO LA MAASKOFU NA WACHUNGAJI KUTOKA MADHEHEBU MBALIMBALI JUU YA TUKIO LA ASKOFU GWAJIMA.
Sisi maaskofu na wachungaji kutoka makanisa mbalimbali tumeshtushwa na kusikitishwa kwa taarifa ya ugonjwa wa Askofu na mtumishi mwenzetu Josephat Gwajima ambaye tarehe 27/03/2015 alifika kituo cha polisi cha kati kuitikia wito wa polisi uliomtaka kwenda kujibu shutuma za kutumia lugha ya matusi kwa kardinali Pengo.
Tumepata fursa ya kutafakari na kujadili kwa kina hali iliyompata Askofu mwenzetu hasa baada ya kuzingatia kuea Askofu Gwajima alifika polisi akiwa mzima na mwenye afya njema lakini wakati wa akihojiwa na polisi, hali yake ilibadilika ghafla kiasi cha kupelekea yeye kulazwa hospitali ya TMJ akiugua tena kwenye wodi ya wagonjwa mahututi yaani (ICU) katika chumba cha uangalizi maalum.
Maswali yetu makuu ni kitu gani kimempata mwenzetu? Tunajiuliza, je vyombo vya usalama vimekua sio sehemu salama kama zamani?
Tukiwa bado tunatafakari hill, tumeshtushwa tena baada ya kupata taarifa ya kuwa Wachungaji Wasaidizi wa Askofu Gwajima pamoja na walinzi wake waliokuwepo hospitalini hapo kwa ajili ya kumuuguza nao pia wamekamatwa kwa tuhuma za. kutaka kumtorosha Askofu Gwajima. 
Jambo hili linashangaza zaidi maana wachungaji wale wale waliokuwa naye akiwa mzima wa afya wakati anaelekea polisi ndio wale wale wanatuhumiwa kutaka kumtorosha akiwa mgonjwa.
Ni jambo la kushangaza na lisiloingia akilini kuwa wasaidizi hao wa Gwajima walitaka kumtorosha wakati Gwajima kama angekua na nia hiyo angekwisha fanya hivyo mana alikuwa na uwezo wa kutoroka alipokua Arusha kwenye kikao cha Maaskofu wakuu wa makanisa ya Kipentekoste ambao alipata taarifa za kuitwa Polisi.
Isitoshe Gwajima aliitija wito na kwenda polisi mwenyewe kwa miguu yake bila kushurutishwa, wala hakufikishwa polisi kwa nguvu.
Swali: Kama alikua anaona ugumu wa kutoroka wakati hakuna polisi anayemlinda na huku akiwa mwenye afya tele, itakuaje rahisi kutoroshwa leo akiwa mahututi na akiwa kwenye ulinzi mkali wa polisi?
Mbona hii inastaajabisha?
Jambo jingine linalotupa shida ni kuhusu mlalamikaji wa kesi hii inayomkabili Askofu Gwajima. Tumeelezwa na wasaidizi wa Askofu Gwajima kuwa pale polisi walielezwa kuwa aliyefungua kesi hii sio Pengo ila mtu mmoja aitwaye Aboubakar.
Kwa ufahamu wetu juu ya sheria unatutuma kuamini kuwa Aboubakar sio MTU sahihi wa kufungua kesi hiyo sababu hawezi kutuonyesha ameumizwa kiasi gani na matamshi ya Askofu Gwajima.
Isitoshe, Kardinali Pengo mwenyewe ametamka katika Ibada yake ya Jumapili hii ya tarehe 29/03/2015 kuwa amemsamehe Gwajima, yupi tena mwenye uchungu wa kumzidi Kardinali Pengo?
RAI YETU:
Rai yetu ni kwamba, ni vizuri serikali pamoja na vyombo vyake vya usalama vikatumia weledi katika kushughulikia mambo ya kidini na viongozi wake kwani yanaweza kusababisha chuki dhidi ya serikali na pia kupelekea mpasuko mkubwa wa kidini katika jamii yetu iliyo na historia nzuri ya umoja na mshikamano na ushirikiano katika matukio yote ya kimaisha.
Tunaomba serikali isaidie kuondoa mkanganyiko huu na busara kubwa itumike ili kuepusha uvunjifu wa Amani katika jamii.
MAAMUZI YETU:
Jambo hili linazungumzika, maana hata hivyo tumeshaazimia kukutana na IGP ili kupata suluhisho juu ya jambo hili.
Kwa niaba ya maaskofu na wachungaji:
Mwenyekiti: Askofu Dr. Mgullu Kilimba
Katibu: Askofu Dr. Dramas Mukassa
Na mwandishi
F.A.K
30/03/2015
[Continue Reading]

BREAKING NEWZZ.....ASKARI WAWILI WAUWAWA NA MAJAMBAZI HUKO KONGOWE


Askari wawili wameuawa jana jioni na majambazi huko Kongowe, nje kidogo ya Jiji la Dar
- Inadaiwa mmoja wa majambazi hao alikuwa na panga ndo akampiga askari aliyekuwa na silaha panga la kisogoni askari akazimia na huyo jambazi kuchukua hiyo silaha akafanya mauaji hayo ya askari wawili
[Continue Reading]

Wednesday, February 18, 2015

MTOTO SOPHIA ANAOMBA MSAADA ILI AWEZE KUPATA MATIBABU

 Sophia Abdul (14)
-----------------
 Na Amon Mtega -  Songea
MTOTO Sophia Abdul (14) anayesoma shule ya msingi Lilahi darasa la tano iliyopo kata ya Mhukulu wilaya ya Songea vijijini mkoani Ruvuma amekumbwa na ugonjwa usiofahamika ambao umejitokeza kwenye  jicho lake  la kulia lililo vimba na kutokezea nje hali inayomletea maumivu makali na kushindwa kwenda shule huku akiomba msaada kwa wasamalia wema.

 Akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za elimu za wilaya hiyo mama wa mtoto huyo Joyce Nyoni alisema kuwa mwanae alianza kupatwa na ugonjwa huo toka Aprili mwaka jana lilianza  kuwasha kisha kujitokeza uvumbe ambao umepelekea jicho hilo kushindwa kuona huku likiwa limetoka kwa nje.

 Alisema baada ya kuona hali ya mwanae inazidi kuwa mbaya alimpeleka katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma na kukutana na madaktari ambao walimwambia kuwa ugonjwa huo hawatauweza badala yake walimtaka atafute fedha ampeleke katika hospitali ya rufaa ya Muhimbili.

Joyce aliongeza kuwa baada ya kupata maelekezo ya madaktari aliamua kupita kuomba msaada kwa wasamalia wema ili kunusuru maisha ya mwanane kwa kuwa yeye mwenyewe hana uwezo wa kifedha na kwamba baba wa mtoto huyo Abdul Rashid alimtelekeza toka akiwa na umri wa mwaka mmoja.

Alisema kufuatia hali hiyo mwanae hajahudhulia masomo toka walipofungua shule jambo ambalo linaweza kumrudisha nyuma katika maendeleo yake na haki ya kupata elimu,hata hivyo aliambiwa na madaktari hao kuwa pindi atakapopata fedha za matibabu watamwandikia kibari cha kumruhusu kwenda kupata matibabu Muhimbili.

Aidha mama wa mtoto huyo anawaomba wasamalia wema kutoa mchango wao wa hali na mali ili afanikiwe kumpeleka mwanae kwenye matibabu kiwango cha fedha kinachohitajika hadi sasa hajafahamu baada ya kupewa kibali atafahamishwa kwa watakao guswa na tatizo la mtoto Sophia watoe michango yao kwa simu namba 0683115075 ya mama yake.
[Continue Reading]

Tuesday, January 20, 2015

MWANAMKE AKAMATWA KWA UNGA WA BIL.2 NYUMBANI KWA MBUNGE Posted By BONGO TIME



MWANAMKE mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Doreen John Mlemba, mwenyeji wa Same mkoani Kilimanjaro, mwishoni mwa mwaka uliopita alikamatwa kwa kuhusishwa na shehena ya madawa ya kulevya aina ya Heroin, yenye thamani ya shilingi bilioni 2.5.
Madawa hayo yalikutwa kwenye nyumba moja iliyopo eneo la Ununio, Tegeta jijini Dar es Salaam, ambayo ni mali ya Mbunge wa CCM (Jina linahifadhiwa) wa jimbo moja la mikoa ya Kanda ya Ziwa, Uwazi limefukunyua.
Taarifa toka vyanzo mbalimbali makini, zinasema majirani wa nyumba hiyo walikuwa na mashaka na kinachofanyika ndani ya nyumba hiyo, kwani licha ya ukubwa na kukamilika kwa ujenzi wake, lakini haikuwa ikikaliwa na mtu na mara chache, watu walionekana wakiingia na kutoka bila kujulikana walichokuwa wakikifanya.
Kutokana na hali hiyo ya wasiwasi, wasamaria wema walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ambalo liliifanyia kazi habari hiyo na kufika kwenye nyumba hiyo na kujaribu kugonga lakini bila mafanikio yoyote.
“Baada ya kugonga, ndipo polisi hao walipoamua kuvunja mlango na kufanya upekuzi katika sehemu zote ndani ya nyumba hiyo, ambapo walifanikiwa kulikuta sanduku ambalo baada ya kufunguliwa, zikagundulika kilo 35 za madawa ya kulevya aina ya Heroin,” kilisema chanzo chetu kilichoshuhudia zoezi hilo.
Kamanda wa Kikosi Cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini, SACP Godfrey Nzowa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa baada ya kukamata shehena hiyo, vijana wake walijikuta katika wakati mgumu wa kumjua mmiliki wa nyumba hiyo.
Hii ni nyumba aliponaswa mwanamke huyo akiwa na unga.
Baada ya kutafuta nyaraka mbalimbali, hatimaye waligundua kuwa nyumba hiyo inamilikiwa na mbunge huyo wa zamani ambaye alitafutwa na kuhojiwa kwa saa kadhaa, ambapo alikiri kuimiliki, lakini akidai kwa muda huo, alikuwa ameipangisha kwa watu aliowataja, bila kujua shughuli iliyokuwa ikifanyika ndani yake.
Inadaiwa kuwa baada ya kupata ushirikiano huo kutoka kwa mbunge huyo, askari waliingia mtaani kuwasaka wapangaji hao, ambapo Septemba 15, mwaka jana, saa saba mchana, walifanikiwa kumkamata Doreen, akiwa shambani kwake, eneo la Ruaha Mbuyuni mkoani Iringa alikokuwa akivuna vitunguu, bamia na bilinganya.

“Tulifanya uchunguzi na tayari watu watano wameshakamatwa akiwemo Doreen, nyumba hiyo waliifanya kama ghala la kuhifadhia madawa na mtu mmoja bado tunaendelea kumsaka, baadhi ya waliokamatwa tulikuwa tukiwasaka kwa muda mrefu,” alisema Kamanda Nzowa.
Aliwashukuru wananchi kwa ushirikiano wao na kuwaomba waendelee hivyo na kwamba donge nono litatolewa kwa watakaofanya hivyo huku majina yao yakihifadhiwa.Gazeti hili lilimfikia Mbunge huyo mmiliki wa nyumba kwa njia ya simu, lakini alikataa kulizungumzia suala hilo, akidai liko chini ya polisi.
“Naomba suala hili umuulize Kamanda Nzowa, mimi siwezi kulizungumzia kwa vile lipo chini ya uchunguzi wao, pamoja na kwamba nawatambua hao wapangaji lakini siwezi kusema lolote,” alisema.
[Continue Reading]

Monday, January 19, 2015

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA MAMLAKA YA HALI YA HEWA NCHINI:: MVUA KUBWA INATEGEMEWA KUNYESHA MIKOA YA PWANI, RUVUMA NA MOROGORO


Leo Mamlaka ya hali ya hewa Imetoa taarifa kwa Umma kuwa Kuanzia Januari 18, 2015 Mpaka Januari 20, 2015 Kunategemewa kutokea Mvua Kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24, Maeneo ambayo yanatarajiwa kuhusika ni Maeneo ya Mikoa ya Ruvuma, Mtwara, Lindi, Morogoro, Pwani, Dar es Salam na Kisiwa cha Unguja.

Sababu za Mvua hiyo ni Kuimarika kwa Mgandamizo mdogo wa Hewa katika Eneo la Bahari ya Hindi mashariki mwa kisiwa cha Madagasca na Hivyo kusababisha ongezeko la unyevunyevu kutoka misitu ya Kongo kuelekea maeneo tajwa hapo juu.

Mamlaka Imetoa angalizo kuwa wakazi wa maeneo yaliyotajwa hapo juu na Mamlaka zinazohusika na Maafa wanashauriwa Kuchukua hatua stahiki.

Pia imesisitiza Inaendelea Kufuatilia hali hiyo na itatoa mrejesho pale itakapobidi.
[Continue Reading]

Thursday, November 13, 2014

Roma Mkatoliki Afunguka ‘Asikwambie Mtu Hakuna Watu Wenye Stress Kama Wasanii’

Lawama‬ zinakuwa nyingi sana naona!!! Na wengi mnazipeleka eneo moja tu!!
Askwambie mtu hakuna watu wenye ‪#‎Stress‬ kama sisi ‪#‎wasanii‬ aaaf mbaya zaidi sisi wengi wetu hatuwezi kuishinda hiyo ‪#‎Challenge‬ finally tunafail!!
Kuna kipindi msanii unakuwa ‪#‎Juu‬ sana na hiyo inatokana na juhudi zako na support unayopewa na wadau wa mziki (media sanasana) na mashabiki!! ‪#‎HALAFU‬ GHAFLA FROM NOWHERE ULE UJUU UNAANZA KUPUNGUA KISHA UNAISHA KABISA!! AU KUNA WAKATI HUO UJUU HAUISHI TARATIBU UNAISHA GHAFLA TU VUUUP!! #STRESS INAANZA!!
SWALI NI KWANINI HUO UJUU UNAISHA GHAFLA!!?
Je uwezo wako unaisha?
Unaridhika mafanikio?
Unaikosa ile support ya awali toka kwa wadau?
Je unashushwa kwa nguvu za watu fulani?
Kuna wengine sasa wasanii wanakuwa hawajawahi kuwa #JUU Lakini wanafight kufika juu na wanajituma hasa na ‪#‎NI_WAKALI‬ sana lakini zinatokea tu ‪#‎FIGISUFIGISU‬ msanii anakuwa hatoboi!! Finally anaamini anabaniwa na hapewi support. ..#STRESS INAANZA!!
Wasanii kama ‪#‎GEEZMABOV‬ tunao wengi sana hapa ‪#‎TANZANIA‬ lakini hatujifunzi kwa mifano!!
kuna vipaji havipaswi kupuuziwa hata kidogo jamani vipeni support a hundred please!! Hatatokea msanii kama ‪#‎AfandeSelle‬ mi nakwambia hadi leo ni mkali sana huyu mtu!! Hakuna ‪#‎Rapper‬ kama ‪#‎JosMtambo‬ askwambie mtu!! Yule ‪#‎Enika‬ yule ni anaimba jamani acha tu!! Hawa vijana wa ‪#‎TamaduniMusic‬ ni new ‪#‎faces‬ zinazokuja vizuri sana wapewe ‪#‎support‬!! ‪#‎Joslin‬#MBDog# hawa watu ni ‪#‎Almasi‬ jamani!! Tunawasanii wakali kibao mi nakwambia ‪#‎DojoNaKaya‬ ni ‪#‎nyoko‬!! Wataimba wote ila mtu kama ‪#‎RamaDee‬ ni hadithi nyingine ujue!!!
Na isiwepo hii hali ya kwamba
“ILI ATOBOE FLANI BASI LAZIMA FLANI APOTEE!! HII KAULI HAINA MASHIKO KIUKWELI!!! Kwanini apotee?? Si tuwe wote tu!!! Na msitetee kwa kusema HATA MAREKANI IKO IVO…kwani si wao!!
Ni lazima tuwaige kwani!!?
ILA UPANDE WA PILI SASA
Lakini wakati mwingine sisi wasanii tuna makosa kutokana na ‪#‎ATTITUDE‬ zetu…tutambue kuwa tunaofanya nao kazi ni ‪#‎WAFANYABIASHARA‬ na sio ndugu zetu wala hakuna sehemu iliyoandikwa NI LAZIMA WAKUSUPPORT!! Kila mtu ana matakwa yake kama mfanyabiashara kama mdau!! So ‪#‎JIONGEZE‬!!
Tuna ‪#‎Angle‬ moja tu sasa ya biashara ya muziki wetu nayo ni ‪#‎SHOW‬
Sasa kuna wasanii unapita #Mwaka hawajapata show na ni wakali sana…na mbaya zaidi bado hawapati #AIRTYM katika media houses!!#WANAUMIA SANA!!!!!
Kama hiyo haitoshi msanii ana miezi 6 hajapata show wala akiaandaa mwenyewe mashabiki hawamsupport anafail…kisha anaskia msanii mchanga tu ametoka juzi amepigiwa simu ya show #MILIONI3 Amekataa!!
Wakati yeye anaitafta hata show ya #LAKI3 tu hapati!! #STRESS INAANZA!!
Finally ukishindwa kui control stress basi uta end up into
NEGATIVE SIDE!!!
Wito wangu tafadhali tuwasapoti na tuzidi kuwasapoti vijana wetu wenye vipaji…najua wapo wenye matatizo lakini tusiikate tamaa tuzidi kuwaonyesha njia bora ya mafanikio…hii ni kwenu mashabiki na wadau wa muziki wetu huu pendwa wa BONGOFLAVA
[Continue Reading]

Tuesday, October 28, 2014

CHIDI BENZ APANDISHWA KIZIMBANI LEO,AKOSA DHAMANA NA KWENDA SEGEREA

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chid Benzi’ leo amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la matumizi ya dawa za kulevya.

Chid Benzi, alipandishwa kizimbani majira ya saa nane mchana, mbele ya Hakimu Warialwande Lema, ambaye alimtaka msanii huyo atolewe nje kutokana na uvaaji mbaya wa suruali yake kwani alivaa ‘Kata kei’ ili avae vizuri nguo.

Akisomewa mashitaka yake, na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono, alidai kwamba mnamo 24 Oktoba 2014, Chidi Benzi alikutwa na dawa hizo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Alidai kwamba, shitaka la kwanza linalomkabili ni kukutwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya sh.38, 638. Pia shitaka la pili ni kukutwa na gramu 1.72 za dawa kulevya aina ya Bangi yenye thamani 1,720.

Mbali na hilo, shitaka la tatu ni kukutwa na vifaa vinavyotumika kuvutia dawa hizo za kulevya, ambapo alikutwa na Kifuu cha nazi kitupu na kijiko kimoja.

Hata hivyo, wakili huyo alidai kwamba upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika. Hakimu Lema alihairisha kesi hiyo hadi Novemba 11, mwaka huu baada wadhamini kushindwa kujitokeza kwa haraka.

Hakimu Lema alisema, mshitakiwa huyo anatakiwa kudhaminiwa na wadhamini wawili wa kudumu pamoja na bonfdi ya Sh.milioni 1.

Hali hiyo ya kushindwa kupata dhamana ilizua hali ya simanzi kwa familia yake, kutokana na kuchelewa kujitokeza kwa wadhamini wake mbele ya Hakimu na hivyo kushindwa kupata dhamana.

Chidi Benzi alikamatwa na dawa za kulevya katika hatua ya ukaguzi kwaajili ya kupanda ndege ya Fastjet akielekea jijini Mbeya, juzi jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

 Msanii wa Hip Hop, Rshid Makwiro ‘Chidi Benzi’ akisindikizwa na askari Polisi wakati akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini leo Dar es Salaam kujibu mashtaka matatu likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)

 Msanii wa Hip Hop, Rshid Makwiro ‘Chidi Benzi’ akiingia Mahakamani leo.

 Chidi Benzi akiwa chini ya ulinzi wa askari Polisi.

Msanii wa Hip Hop, Rshid Makwiro ‘Chidi Benzi’ akisindikizwa na askari Polisi wakati akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana kujibu mashtaka matatu likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 

 Chidi Benzi akipanda karandinga kwa ajili ya kuelekea katika mahabusu ya Segerea.
[Continue Reading]

Saturday, October 25, 2014

MANENO MAZITO KUTOKA KWA RAY C KWENDA KWA CHID BENZ BAADA YA KUKATWA NA MADAWA YA KULEVYA

“Pole kaka yangu Chidi Benz,Naumia kuona tatizo uliokuwa nalo bado haujalitaftia jibu unalijua la kutatua tatizo lako,Mimi ni dada yako na tumeshafanya kazi Pamoja,Tatizo ulilonalo na Mimi nilishakuwa nalo na niliweza kulitatua sababu nilijitambua na kutafuta suluhu,nimejaribu kila njia kukushauri badala yake ukaja na rungu la kimasai na kunitandika nalo nyumbani kwangu!nadhani janga hili lililokukuta litakuwa Kama jibu kwako kwamba unakoenda si salama kabisa kaka yangu ni bora ubadilishe njia ili uweze kuungana nasi kwenye tiba ya Methadone kwani ndio Kiboko ya madawa ya kulevya!!!!Kama Mimi mwanamke nimeweza najua Hata wewe utaweza!!!!Tanzania bila madawa ya kulevya Inawezekana !!Watanzania tusimyanyapae Msanii wetu kwani Uteja ni ugonjwa Kama ugonjwa mwingine na Unazuilika na Kutibika,Ana kipaji na Ana uwezo wa kurudi tena kwenye Sanaa,Tumuombee mema………Tanzania Stand Up n Wish Him Luck…………With Love,Ray C Foundation.”
[Continue Reading]

Friday, August 8, 2014

KIJANA WA MIAKA 19 ANAVYOTESEKA KWA UGONJWA WA AJABU

ANAITWA NURDIN LULANGA AMEZALIWA MWAKA
1990 DAR ES SALAAM TANZANIA , HIVYO ANA
MIAKA 19 .HISTORIA YA UGONJWA HUU ILIANZA
WAKATI KIJANA HUYU AKIWA DARASA LA 6
( SITA NA ILIKUWA NI MAUMIVU YA KAWAIDA TU
YA MGUU JUU YA GOTI NA INAFIKIA MDA
MWINGINE ANASHINDWA HATA KUTEMBEA .
MAUMIVU HAYO YALIKUWA YANAENDELEA NA
KUACHA NA BAADA YA MDA UKAANZA KUVIMBA
TARATIBU NA BAADA YA KWENDA KUCHUKUA
VIPIMO VYA X -RAY IKAONEKANA KAMA MFUPA
ULIKUWA UNALIKA TARATIBU .
BAADA YA KUFIKA FORM SIX TERM
YA KWANZA MGUU ULIVIMBA GHAFLA KWA KASI
YA AJABU NA NDIO IMESABABISHA ASHINDWE
KABISA KUTEMBEA HUU SASA NI MWENZI WA 9
YUKO TU NYUMBANI . AMESHAPIMA FULL BLOOD
PICTURE,ABSOMEN , BONE SCAN ( OCEAN ROAD )
N. K
LAKINI HAKUNA KIPIMO KILICHOONYESHA
DIRECT ANAUMWA UGONJWA GANI MADAKTARI
WAMETUSHAURI TUMPELEKE NJEE YA NCHI NA
FAMILIA HAINA UWEZO HUO JAMANI NDUNGU
WATANZANIA TUNAOMBA MSAADA WENU ILI
TUMSAIDIE HUYU KIJANA KATIKA UGONJWA
HUUNATANGULIZA SHUKURANI ZANGU ZA DHATI
KWA YEYOTE ATAKAE GUSWA NA HILI TATIZO ANAWE ANAWEZA AKATUMA CHOCHOTE ULICHO NACHO KUPITIA NAMBA 0758153308 KUTOA NI MOYO NA SI UTAJIRI
Ally Kiba Tz's photo.
Ally Kiba Tz's photo.Ally Kiba Tz's photo.
[Continue Reading]

Friday, July 11, 2014

ANAOMBA MSAADA WAKO ASIENDELEE KUOZA MGUU

kijana Peter  Sitiwati akiwa na maumivu makali yaliyosababishwa na kuoza kwa mguu.
 AMA kweli ng’ombe wa maskini hazai, kijana Peter  Sitiwati (26), mkazi wa Sinza ya kwa Remmy jijini Dar amejikuta akikatisha ndoto za utafutaji maisha kufuatia kuoza mguu baada ya ajali mbaya ya gari.Akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar juzi kati kwa sauti ya kukata tamaa, Peter alisema alipata ajali ya gari mwaka 2013 maeneo ya Sinza-Mori, Dar na kuumia vibaya mguu wa kulia.’’Baada ya kugongwa na gari niliangukia mtaroni nikachomwa na kijiti kwenye mguu wa kulia. Nilikimbizwa Hospitali ya Palestina kutibiwa na baada ya muda mguu ulionesha kupona kwa juu, lakini kumbe ndani kidonda kilikuwa kibichi na kiliendelea kulika bila mimi kujua.
 “Mwanzoni mwa mwaka huu (2014) nikaanza kushangaa usaha mwingi unatoka sehemu mbalimbali ya mguu tena na harufu mbaya, mguu ukaonekana umeoza tena una matundu matatu, si unauona ulivyo, hata watu hawapendi kukaa jirani na mimi,” alisema Peter huku akionesha mguu wake huo.



Muonekano wa mguu wa Peter  Sitiwati.

 Peter alisema atashukuru kama atapata nauli ya kurudi kwao, Makambako, Njombe kwa vile ameona maisha magumu huku akiishi kwa kushindwa kula na kulala kwa shida.
 “Ila namshukuru sana msamaria mwema anaitwa Louis, ndiye anayenisaidia kwa sasa,” alisema.

Aliongeza kuwa, baada ya kuhangaika kusaka nauli bila mafanikio, baadhi ya watu walimwambia atoe taarifa kwenye Magazeti Pendwa ya Global Publishers ambayo yanasomwa na watu wengi Tanzania, atasaidiwa.
 “Napenda kuwaomba Watanzania mnaosoma Magazeti Pendwa ya Shigongo mnichangie pesa ili nipate matibabu na nauli ya kurudi  kwetu. Wenye kuguguswa na tatizo langu wanaweza kunisaidia kwa kutumia namba ya simu 0716 122 780,  Louis.
[Continue Reading]

AJALI YAUA MMOJA DODOMA, MWANAMKE AGONGWA NA KUFARIKI PAPO HAPO

 Watu wakiuangalia mwili wa mtu ambaye hakufahamika jina jina lake baada kugongwa na gari lisilofahamika na kufa papo hapo, katika eneo la bohari ya mkoa kati ya bunge na kituo cha mabasi yaendayo mikoani, barabara ya Morogoro - Dodoma.


 Polisi wa usalama barabarani wakisaidiana na wananchi kuupakia mwili wa mtu aliyekutwa amegogwa na kufa papo hapo na gari ambalo halikujulikana baada ya kukimbia katika barabara ya Morogoro - Dodoma karibu na jengo la bunge la Tanzania. 
Na John Banda, Dodoma

MWANAMKE asiyefahamika wa umri wa makamo amepoteza maisha baada ya kugongwa na gari aina ya Coster linalofanya shughuli za Daladala kati ya Udom Nanenane ambalo halikufahamika namba zake za usajili na kisha Gari hilo kutokomea kusikojulikana.
Kwa mujibu wa mashuhuda walioshudia tukio hilo wamesema majira ya saa 2. 30 walishuhudia kishindo kikubwa Barabarani eneo la Bohari karibu na kipitashoto kilichopo kituo cha mabasi yaendayo mikoani mjini Dodoma, ambapo baada ya kishindo hicho gari hilo liliendelea na safari zake. Mmoja wa mashuhuda hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Baraka amesema hakumuona mtu huyo wakati anavuka bali aliona Costaer hiyo mita chache kabla ya kusikia kishindo hicho na kilichomfanya ajue kuwa
ni mtu kagongwa ni kutokana na gari la nyuma kumulika mwanga ndipo alipoona tairi ya nyuma ikimalizikia kumkanyaga na kufa hapohapo.
Mkaguzi wa polisi wa usalama Barabarani Methew Mtakije  aliyefika kushuhudia tukio hilo alisema tukio hilo lilisababishwa na mwendo kasi wa Dereva wa gari hilo ambaye alikiuka sheria za usalama barabarani ambazo zinamtaka kila dereva kuendesha spidi 50 kwa saa wanapokuwa
mijini.
MtakijaAmesema mwendo kasi ni hatari  wakati wowote hasa nyakati za usikukutokana na muono mdogo unaosababishwa na giza hivyo madereva wotewazingatie sheria zilizopo ili waweze kuepusha ajili, na kuahidi kulisakagari hilo mpaka kulipata. Mwili wa Marehemu huyo ambae bado hajafahamika umehifadhiwa katika chumba cha maiti kilichopo katika hospitali yamkoa wa Dodoma.
[Continue Reading]

Thursday, July 10, 2014

MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR'AN TUKUFU YA TAIFA 2014 - AISHA SURURU FOUNDATION

 Aisha Sururu Foundation inawataarifu fainali ya mashindano ya kuhifadhi Qur'an takatifu ya taifa ya mwaka 2014 yatafanyika Jumamosi hii ya tarehe 12/07/2014 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Hall ambapo vijana wanawake na waume walioshiriki katika mashindano hayo watapigania nafasi zao za kwanza mbele ya umma na wageni waalikwa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.

Mwaka huu Aisha Sururu Foundation imeshirikisha mikoa 9 ya Tanzania ikiwemo visiwa vya Zanzibar na Pemba ambapo vijana watakaoshiriki kutoka visiwa vya Pemba ni vijana walemavu wa macho, walemavu wa viungo na kadhalika. Njoo uje ushuhudie uwezo wa Allah (Mwenyezi Mungu) vipi walemavu wa macho na vijana wengineo walivyojiwezesha kufika kwenye jukwaa la mashindano ya kuhifadhi Qur'an ya taifa ya mwaka 2014.

Uongozi wa Aisha Sururu Foundation unawaalika Watanzania wote waje pamoja kushuhudia mashindano haya na kuwashajiisha vijana wote walioshiriki katika mashindano haya ya taifa ya mwaka 2014.

Ukumbi wa Diamond Jubilee Hall
Tarehe 12/07/2014, Jumamosi
Kuanzia saa tatu asubuhi (9am) mpaka saa nane mchana (2pm)

Wabillahi tawfeeq,


Ramadhan Mubaarak,
[Continue Reading]

RAIS KIKWETE AVUTIWA NA NGUO ZINAZOTENGENEZWA NA KAMPUNI YA BINTI AFRICA UNIQUE COLORFUL QUALITY

Rais Jakaya Kikwete akichagua mashati yaliyomvutia kwa ubora yanayotengenezwa na Kampuni ya Binti Africa Unique Colorful Quality ya Jijini Dar es Salaam akiongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu na Meneja mwa na mitindo, Johari Kemmy Sadiq (kushoto), Rais alitembelea banda la Binti Africa kwenye Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yaliyomalizika juzi.Wengine Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda wa pili kulia.


RaisJakayaKikwete (pili kulia) akichagua mashati yaliyomvutia kwa ubora yanayotengenezwa na Kampuni ya Binti Africa Unique Colorful Quality ya Jijini Dar es Salaam akiongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu na Meneja mwanamitindo, Johari Kemmy Sadiq (wa pili kushoto), Rais alitembelea banda la Binti Africa kwenye Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yaliyomalizika juzi. Wengine Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Jacqueline Maleko na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mushi (katikati)
[Continue Reading]

Tuesday, July 8, 2014

MTOTO MIAKA 3 AJISAIDIA HAJA KUBWA KWA NJIA YA MDOMO

MASKINI Mungu wangu! Ndiyo maneno aliyoanza nayo kusema mama mzazi wa mtoto Salome Abdallah Said (3), kutokana na mwanaye huyo afya yake kuzidi kubadilika kufuatia kuumwa mara kwa mara licha ya kufanyiwa upasuaji mara mbili.
Mtoto Salome Abdallah Said (3) akiwa na kovu tumboni baada ya upasuaji.
Akizungumza na gazeti hili wiki iliyopita mama wa mtoto huyo Veronica Laurent, mkazi wa Bunju B, jijini Dar es Salaam alisema kwamba mwanaye kwa sasa hali yake siyo nzuri kwa vile amekuwa akijisaidia haja kubwa kupitia mdomoni kama hapo awali, hali hiyo anasema ameambiwa na madaktari inasababishwa na utumbo wake wa haja kubwa kujikunja.
Muonekano wa karibu wa kovu la Salome Abdallah Said.
HISTORIA YA MTOTO
Veronica anaeleza: “Mwanangu kwa sasa ana miaka mitatu, tangu nimzae katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar, aligundulika ana matatizo ya kutojisaidia haja kubwa kama kawaida ilibidi nipelekwe Hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
“Nilimfikisha Muhimbili akiwa katika hali mbaya akawa anajisaidia haja kubwa kupitia mdomoni, hata hivyo, nikaambiwa tumpeleke Hospitali ya Agha Khan kwa vipimo zaidi, huko akagundulika kuwa utumbo wa haja kubwa umejikunja.”
Mtoto Salome Abdallah Said akiwa na mama yake.
AFANYIWA UPASUAJI MUHIMBILI
Katika maelezo yake mama huyo alisema kwamba mtoto wake alifanyiwa upasuaji kwa mara ya kwanza tumboni na kuwekwa tundu ambalo alikuwa akilitumia kutolea haja kubwa, baadaye akafanyiwa tena upasuaji kwa mara ya pili chini ya tumbo na kuwekewa utumbo bandia lakini hata hivyo, ulikuwa mwembamba hivyo ukawa haufanyi kazi vizuri.
UTUMBO WA BANDIA
“Tulipotoka Muhimbili na kurejea nyumbani haikuchukua siku nyingi hali ya mtoto ikazidi kuwa mbaya, akawa analia kila mara nikaamua kurudi Muhimbili.
“Madaktari baada ya uchunguzi wakasema utumbo wa bandia aliowekewa ulikuwa mdogo na mwembamba hivyo ulishindwa kufanya kazi pia utumbo ulikuwa umejikunja.
“Niliambiwa zinahitajika shilingi laki tisa ili afanyiwe matibabu ambapo nimeshindwa kuzipata, bora awamu ya kwanza alijitokeza mdhamini akatoa shilingi laki tisa. Nawaaomba Watanzania wenzangu wamsaidie mwanangu ili kumnusuru na kifo, maana madaktari wamesema bila kufanyiwa hivyo anaweza kupoteza maisha,” alisema mama huyo.
Akifafanua zaidi alisema: “Wakati fulani ili apitishe haja kubwa katika njia ya kawaida inabidi ninunue dawa ya kulainisha kinyesi kwani bila kufanya hivyo ni lazima ajisaidie kwa kupitia mdomoni.”
BABA YAKE ATOROKA
“Kwa sasa mtoto halali kutokana na kulia kutokana na maumivu makali, baba yake baada ya kuona tatizo la huyu mwanangu alitoweka na kuzima simu, hapatikani. Mimi nashindwa kufanya kazi yoyote.
Nawaomba Watanzania mnisaidie kupitia namba yangu ya simu 0712 004 677 au 0767 026 551,” alisema mama huyo huku akilengwalengwa na machozi.
[Continue Reading]

ARUSHA TENA....! WATU NANE WANADAIWA KUJERUHIWA VIBAYA NA BOMU NDANI YA MGAHAWA



  Pichani ni Askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ kitengo cha Mabomu wakiwa katika eneo la tukio ambapo bomu lilirushwa ndani ya Mgahawa ujulikanao kwa jina la Traditional Indian Cusine uliopo pembeni ya hotel ya Gymkana jijini Arusha,aidha taarifa za awali zinaeleza kuwa watu nane wamejeruhiwa vibaya na mlipuko huo .

 Picha ni majeruhi wa mlipuko wa Bomu uliotokea katika mgahawa wa Traditional Indian Cusine aliyejulikana kwa jina la Deepak Gupta (25),akiwa amelazwa katika hospitali ya Selian,katika chumba cha watu mahututi (ICU),mara baada ya kukatwa mguu wake mmoja wa kushoto kutokana na mhuu huo kujeruhiwa vibaya na bomu.


 Sehemu ya baadhi ya watu waliojeruhiwa kwenye mlipuko wa bomu uliotokea jana usiku katika mgahawa wa Traditional Indian Cusine wakiwa wamelazwa katika hospitali ya Selian,jijini Arusha kwa matibabu. 


[Continue Reading]
Powered By Blogger · Designed By Seo Blogger Templates