Thursday, July 10, 2014

MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR'AN TUKUFU YA TAIFA 2014 - AISHA SURURU FOUNDATION

 Aisha Sururu Foundation inawataarifu fainali ya mashindano ya kuhifadhi Qur'an takatifu ya taifa ya mwaka 2014 yatafanyika Jumamosi hii ya tarehe 12/07/2014 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Hall ambapo vijana wanawake na waume walioshiriki katika mashindano hayo watapigania nafasi zao za kwanza mbele ya umma na wageni waalikwa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.

Mwaka huu Aisha Sururu Foundation imeshirikisha mikoa 9 ya Tanzania ikiwemo visiwa vya Zanzibar na Pemba ambapo vijana watakaoshiriki kutoka visiwa vya Pemba ni vijana walemavu wa macho, walemavu wa viungo na kadhalika. Njoo uje ushuhudie uwezo wa Allah (Mwenyezi Mungu) vipi walemavu wa macho na vijana wengineo walivyojiwezesha kufika kwenye jukwaa la mashindano ya kuhifadhi Qur'an ya taifa ya mwaka 2014.

Uongozi wa Aisha Sururu Foundation unawaalika Watanzania wote waje pamoja kushuhudia mashindano haya na kuwashajiisha vijana wote walioshiriki katika mashindano haya ya taifa ya mwaka 2014.

Ukumbi wa Diamond Jubilee Hall
Tarehe 12/07/2014, Jumamosi
Kuanzia saa tatu asubuhi (9am) mpaka saa nane mchana (2pm)

Wabillahi tawfeeq,


Ramadhan Mubaarak,

No comments:

Speak Your Mind

Powered By Blogger · Designed By Seo Blogger Templates