kijana Peter Sitiwati akiwa na maumivu makali yaliyosababishwa na kuoza kwa mguu.
AMA
kweli ng’ombe wa maskini hazai, kijana Peter Sitiwati (26), mkazi wa
Sinza ya kwa Remmy jijini Dar amejikuta akikatisha ndoto za utafutaji
maisha kufuatia kuoza mguu baada ya ajali mbaya ya gari.Akizungumza
na mwandishi wetu jijini Dar juzi kati kwa sauti ya kukata tamaa, Peter
alisema alipata ajali ya gari mwaka 2013 maeneo ya Sinza-Mori, Dar na
kuumia vibaya mguu wa kulia.’’Baada
ya kugongwa na gari niliangukia mtaroni nikachomwa na kijiti kwenye
mguu wa kulia. Nilikimbizwa Hospitali ya Palestina kutibiwa na baada ya
muda mguu ulionesha kupona kwa juu, lakini kumbe ndani kidonda kilikuwa
kibichi na kiliendelea kulika bila mimi kujua.
“Mwanzoni
mwa mwaka huu (2014) nikaanza kushangaa usaha mwingi unatoka sehemu
mbalimbali ya mguu tena na harufu mbaya, mguu ukaonekana umeoza tena una
matundu matatu, si unauona ulivyo, hata watu hawapendi kukaa jirani na
mimi,” alisema Peter huku akionesha mguu wake huo.
Muonekano wa mguu wa Peter Sitiwati.
Peter
alisema atashukuru kama atapata nauli ya kurudi kwao, Makambako, Njombe
kwa vile ameona maisha magumu huku akiishi kwa kushindwa kula na kulala
kwa shida.
“Ila namshukuru sana msamaria mwema anaitwa Louis, ndiye anayenisaidia kwa sasa,” alisema.
Aliongeza
kuwa, baada ya kuhangaika kusaka nauli bila mafanikio, baadhi ya watu
walimwambia atoe taarifa kwenye Magazeti Pendwa ya Global Publishers
ambayo yanasomwa na watu wengi Tanzania, atasaidiwa.
“Napenda
kuwaomba Watanzania mnaosoma Magazeti Pendwa ya Shigongo mnichangie
pesa ili nipate matibabu na nauli ya kurudi kwetu. Wenye kuguguswa na
tatizo langu wanaweza kunisaidia kwa kutumia namba ya simu 0716 122
780, Louis.
No comments: