Lawama zinakuwa nyingi sana naona!!! Na wengi mnazipeleka eneo moja tu!!
Askwambie mtu hakuna watu wenye #Stress kama sisi #wasanii
aaaf mbaya zaidi sisi wengi wetu hatuwezi kuishinda hiyo #Challenge
finally tunafail!!
Kuna kipindi msanii unakuwa #Juu sana na hiyo inatokana na
juhudi zako na support unayopewa na wadau wa mziki (media sanasana) na
mashabiki!! #HALAFU GHAFLA FROM NOWHERE ULE UJUU UNAANZA KUPUNGUA
KISHA UNAISHA KABISA!! AU KUNA WAKATI HUO UJUU HAUISHI TARATIBU UNAISHA
GHAFLA TU VUUUP!! #STRESS INAANZA!!
SWALI NI KWANINI HUO UJUU UNAISHA GHAFLA!!?
Je uwezo wako unaisha?
Unaridhika mafanikio?
Unaikosa ile support ya awali toka kwa wadau?
Je unashushwa kwa nguvu za watu fulani?
Kuna wengine sasa wasanii wanakuwa hawajawahi kuwa #JUU Lakini
wanafight kufika juu na wanajituma hasa na #NI_WAKALI sana lakini
zinatokea tu #FIGISUFIGISU msanii anakuwa hatoboi!! Finally anaamini
anabaniwa na hapewi support. ..#STRESS INAANZA!!
Wasanii kama #GEEZMABOV tunao wengi sana hapa #TANZANIA lakini hatujifunzi kwa mifano!!
kuna vipaji havipaswi kupuuziwa hata kidogo jamani vipeni support a
hundred please!! Hatatokea msanii kama #AfandeSelle mi nakwambia
hadi leo ni mkali sana huyu mtu!! Hakuna #Rapper kama #JosMtambo
askwambie mtu!! Yule #Enika yule ni anaimba jamani acha tu!! Hawa
vijana wa #TamaduniMusic ni new #faces zinazokuja vizuri sana
wapewe #support!! #Joslin#MBDog# hawa watu ni #Almasi jamani!!
Tunawasanii wakali kibao mi nakwambia #DojoNaKaya ni #nyoko!!
Wataimba wote ila mtu kama #RamaDee ni hadithi nyingine ujue!!!
Na isiwepo hii hali ya kwamba
“ILI ATOBOE FLANI BASI LAZIMA FLANI APOTEE!! HII KAULI HAINA
MASHIKO KIUKWELI!!! Kwanini apotee?? Si tuwe wote tu!!! Na msitetee kwa
kusema HATA MAREKANI IKO IVO…kwani si wao!!
Ni lazima tuwaige kwani!!?
ILA UPANDE WA PILI SASA
Lakini wakati mwingine sisi wasanii tuna makosa kutokana na
#ATTITUDE zetu…tutambue kuwa tunaofanya nao kazi ni
#WAFANYABIASHARA na sio ndugu zetu wala hakuna sehemu iliyoandikwa NI
LAZIMA WAKUSUPPORT!! Kila mtu ana matakwa yake kama mfanyabiashara kama
mdau!! So #JIONGEZE!!
Tuna #Angle moja tu sasa ya biashara ya muziki wetu nayo ni #SHOW
Sasa kuna wasanii unapita #Mwaka hawajapata show na ni wakali
sana…na mbaya zaidi bado hawapati #AIRTYM katika media houses!!#WANAUMIA
SANA!!!!!
Kama hiyo haitoshi msanii ana miezi 6 hajapata show wala akiaandaa
mwenyewe mashabiki hawamsupport anafail…kisha anaskia msanii mchanga tu
ametoka juzi amepigiwa simu ya show #MILIONI3 Amekataa!!
Wakati yeye anaitafta hata show ya #LAKI3 tu hapati!! #STRESS INAANZA!!
Finally ukishindwa kui control stress basi uta end up into
NEGATIVE SIDE!!!
Wito wangu tafadhali tuwasapoti na tuzidi kuwasapoti vijana wetu
wenye vipaji…najua wapo wenye matatizo lakini tusiikate tamaa tuzidi
kuwaonyesha njia bora ya mafanikio…hii ni kwenu mashabiki na wadau wa
muziki wetu huu pendwa wa BONGOFLAVA
No comments: