Watu
wakiuangalia mwili wa mtu ambaye hakufahamika jina jina lake baada
kugongwa na gari lisilofahamika na kufa papo hapo, katika eneo la bohari
ya mkoa kati ya bunge na kituo cha mabasi yaendayo mikoani, barabara ya
Morogoro - Dodoma.
Polisi wa usalama barabarani wakisaidiana na wananchi
kuupakia mwili wa mtu aliyekutwa amegogwa na kufa papo hapo na gari
ambalo halikujulikana baada ya kukimbia katika barabara ya Morogoro -
Dodoma karibu na jengo la bunge la Tanzania.
Na
John Banda, Dodoma
MWANAMKE
asiyefahamika wa umri wa makamo amepoteza maisha baada ya kugongwa na gari
aina ya Coster linalofanya shughuli za Daladala kati ya Udom Nanenane
ambalo halikufahamika namba zake za usajili na kisha Gari hilo kutokomea
kusikojulikana.
Kwa
mujibu wa mashuhuda walioshudia tukio hilo wamesema majira ya saa 2. 30
walishuhudia kishindo kikubwa Barabarani eneo la Bohari karibu na
kipitashoto kilichopo kituo cha mabasi yaendayo mikoani mjini Dodoma,
ambapo baada ya kishindo hicho gari hilo liliendelea na
safari zake. Mmoja wa mashuhuda hao aliyejitambulisha kwa jina moja la
Baraka amesema hakumuona mtu huyo wakati anavuka bali aliona Costaer
hiyo mita chache kabla ya kusikia kishindo hicho na kilichomfanya ajue
kuwa
ni
mtu kagongwa ni kutokana na gari la nyuma kumulika mwanga ndipo alipoona
tairi ya nyuma ikimalizikia kumkanyaga na kufa hapohapo.
Mkaguzi
wa polisi wa usalama Barabarani Methew Mtakije aliyefika kushuhudia
tukio hilo alisema tukio hilo lilisababishwa na mwendo kasi wa Dereva wa
gari hilo ambaye alikiuka sheria za usalama barabarani ambazo zinamtaka
kila dereva kuendesha spidi 50 kwa saa wanapokuwa
mijini.
MtakijaAmesema
mwendo kasi ni hatari wakati wowote hasa nyakati za usikukutokana na
muono mdogo unaosababishwa na giza hivyo madereva wotewazingatie sheria
zilizopo ili waweze kuepusha ajili, na kuahidi kulisakagari hilo mpaka
kulipata. Mwili wa Marehemu huyo ambae bado hajafahamika umehifadhiwa
katika chumba cha maiti kilichopo katika hospitali yamkoa wa Dodoma.
No comments: