Thursday, November 13, 2014

JONAS MKUDE ASAINI MIAKA MIWILI SIMBA


Hatimaye kiungo Jonas Mkude amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba.
Mkude ambaye ni tegemeo katika kiungo cha ulinzi cha Simba, amesaini mkataba huo leo mbele ya Rais wa Simba, Evans Aveva.
Pamoja na Aveva na viongozi wengine wa Simba akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, Mkude alisaini mkataba huo mbele ya waandishi wa habari. Awali kulikuwa na taarifa kwamba Mkude ameishaongeza mkataba Simba.

No comments:

Speak Your Mind

Powered By Blogger · Designed By Seo Blogger Templates