Showing posts with label MUZIKI. Show all posts
Showing posts with label MUZIKI. Show all posts

Wednesday, July 15, 2015

HUYU YOUNG DEE HEBU ONA ANACHOKIFANYA HAPA


Msanii Young Dee amshika maungio msanii chipukizi Pvcombo,mashabiki wa mfananisha na Wema Sepetu 
video ya nyimbo yake!

 
[Continue Reading]

Tuesday, July 14, 2015

BARAKAH DA PRINCE _CHUKUA MUDA WAKO KUSOMA HAYA MASHAIRI YA WIMBO WA - SIACHANI NAWE


(verse1)
Wakati nalainisha moyo kupenda sio kama ninakosea
ipo sababu ya mimi kurejesha namba ambayo ilipotea
hali ya mtoto kumsusa mama akishachapwa
ni sawa na mapenzi
ukishapendwa
unasahau hata kama ulishafanyiwaga ushenzi
nakumbuka nilijuta sana kupenda kupenda kusikokua na thamani
ila hitaji la moyo lalazimisha kurudia zamani 



(chorus)
mimi bado nina imani
ipo siku utanipa thamani
mimi bado nina imani
jua me siachani nawe
na sishindani nawe
maana upo moyoni ndani
acha nisote mie
ila me siachani nawe
na sishindani nawe
maana upo moyoni ndani
wacha nisote mie

(verse2)
labda juu ya kaburi utanipenda mimi nikiwa sina uhai
hisia zangu haziheshimiwi najidharau sifai
heri ya upofu wa macho
kwa yale nayoyaona
umeruhusu mboni zangu me kumwaga machozi
yaani ungejua hisia za mapenzi
kutesa moyo ila bado hazichoshi
kupendwa sipendwi najua wazi ila bado silingi
maana kesho nitaurubuni moyo
unapendwa na unapenda me meno ila najiona kibogoyo
kweli penzi donda moyo

(chorus)
mimi bado nina imani
ipo siku utanipa thamani
mimi bado nina imani
jua me siachani nawe
na sishindani nawe
maana upo moyoni ndani
acha nisote mie
ila me siachani nawe
na sishindani nawe
maana upo moyoni ndani
wacha nisote mie
[Continue Reading]

WASANII WAIOMBA SERIKALI KUUMALIZIA UKUMBI WA BASATA

Wasanii nchini wameiomba Serikali kumalizia ujenzi wa ukumbi wa Sanaa za maonesho unaojengwa kwa zaidi ya miaka minane sasa makao makuu ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) eneo la Ilala sharif Shamba jijini Dar es Salaam.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa ya Baraza hilo mapema wiki hii, wasanii hao walieleza kwamba kwa sasa kuna ufinyu wa kumbi za za maonesho hali ambayo imekuwa ikiwafanya wasanii hao kukosa maeneo ya kufanya sanaa zao hivyo kumalizika kwa ukumbi huo itakuwa ni ahueni kubwa kwao.

“Ukumbi huu ni muhimu sana kwetu, wengi tuliutazama kama mwanzo wa ufufuaji wa Sanaa za majukwaani lakini sasa ni muda mrefu hauoneshi dalili za kumalizika. Kuna kila sababu ya ukumbi huu kukamilika ili kutusaidia katika maonesho yetu” alisema Msanii Khalid Kambau.

Kwa upande wake msanii wa Sanaa za maigizo Christian Kauzeni ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha wasanii waigizaji mkoani Dar es Salaam alisema kwamba kutokana na ukumbi huo kutazamwa kama mkombozi wa wasanii kuna kila sababu ya kuangalia mbinu mbalimbali ili kuhakikisha unakamilika mapema iwezekanavyo.

Awali akiwasilisha mada kwenye Jukwaa hilo la Sanaa iliyohusu ‘Ubora wa Filamu na Changamoto zake’ msanii na mzalishaji filamu maarufu nchini William Mtitu alisema kwamba tasnia ya filamu chini imepata umaarufu na kukua ingawa bado changamoto za uharamia, elimu na masoko zimeendelea kuiathiri.

“Kwa sasa filamu zinazozalishwa zimekuwa na ubora kuliko huko nyuma. Tatizo liko kwenye elimu kwa wasanii, uharamia na masoko. Kulikuwa na maduka zaidi ya sabini na tano yanayouza kazi za wasanii wa filamu lakini kwa sasa yamebaki sita tu. Wengi wameamua kuuza kazi za nje mbazo ni nafuu. Hii ni hatari” alisisitiza Mtitu.

Aliongeza kwamba pamoja na Serikali kuirasimisha sekta ya filamu bado kuna changamoto ya kazi zinazotoka nje kutokuwekewa stempu za mamlaka ya mapato huku kukiwa na uharamia unaotishia bei za filamu halali zenye stempu hizo.

Jukwaa la BASATA limekuwa likifanyika kwa mwezi mara mbili siku za Jumatatu na wiki hii kulikuwa pia na utambulisho wa asasi ya ubalozi wa Utamaduni wa Mwafrika ambayo imeasisiwa nchini Cameroon, Afrika Magharibi mwaka 2014.
Msanii na mzalishaji filamu nchini William Mtitu (Kulia) akiongea na wadau wa Sanaa (hawako pichani) wakati akiwasilisha mada iliyohusu ‘Ubora katika filamu na changamoto zake’ kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema wiki hii. Kushoto ni Katibu wa chama cha waandishi wa habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) Hassan Bumbuli.
Rais na mwanzilishi wa asasi ya Mabalozi wa Utamaduni wa Mwafrika (African Culltural Embassy Association) Bwana Colpas Numfor kutoka nchini Cameroon (Katikati) akionesha nyaraka mbalimbali za usajili wa asasi yake wakati akiongea na wadau wa Sanaa kwenye programu ya BASATA ya Jukwaa la Sanaa. Kushoto kwake ni Katibu wa chama cha waandishi wa habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) Hassan Bumbuli na Kaimu Mkurugenzi wa asasi hiyo nchini Tanzania Bw. Maganiko Charles.
Msanii maarufu wa Sanaa za majukwaani na maigizo Bakari Mbelemba maarufu kama Mzee Jangala akifuatilia kwa makini mjadala kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema wiki hii. Kushoto kwake ni Rais wa chama cha wacheza bao nchini Bw. Mande Likwepa.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyoibuka kwenye Jukwaa hilo la Sanaa.
Afisa Masoko kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Pastory John akitoa maelezo mbalimbali kuhusu urasimishaji wa sekta ya filamu nchini kwenye Jukwaa hilo la Sanaa.
Mdau wa Sanaa na utamduni Bw. Francis Kaswahili naye alitoa mchango wake kwenye Jukwaa la Sanaa. Alitoa wito kwa wasanii kuhakikisha wanakuwa na kauli moja katika kuhakikisha wanasimamia maslahi yao.
Sehemu ya wadau wa Sanaa waliohudhuria Jukwaa la Sanaa wiki hii.
[Continue Reading]

Wednesday, February 18, 2015

OMMY DIMPOZ AFUNGUKA KUHUSU KUKATALIWA KUINGIA MAREKANI.

Miongoni mwa stori zilizochukua headline kwenye radio mbalimbali, hata kwenye magazeti ni kuhusiana na msanii wa Ommy Dimpoz kuzuiliwa kuingia Marekani na kurudishwa Tanzania bila kufanya show zake.
Sasa basi Kupitia Amplifaya ya Clouds FM Ommy Dimpoz ame amplify na kusema;”…Mimi hata mwenye hizo habari zimenishangaza na kilichonishangaza zaidi stori jinsi zilivyokuja na zilizovumishwa sijui zimekuja vipi kimenishangaza zaidi au unakuta hata mtu ni professional, watangazaji, Waandishi,wengine mtu aandika tu stori au anaongelea stori kwa maana unatengeneza stori kwa kusikia kitu ambacho hauna ushahidi wala haujamsikia mhusika pengine hata kuongea na management yangu, au lakini hata kuongelea ile kuhusu mhusika maana meneja wangu aliniambia ameulizwa imekuaje akawajibu kwamba Ommy ame ni text anarudi leo kwa hiyo yeye atakuwa na majibu yote lakini unakuta stori tu zinaongelewa ambapo hata mimi mwenyewe sijasikilizwa kitu gani kimetokea..” 
Millardayo….. Ilikuwaje? 
Ommy Dimpoz:…”kilichotokea ni kwamba mimi nilitoka hapa nikaenda mpaka Amsterdam na Amsterdam nilikuwa na connect flight kutoka Amsterdam kwenda detroit na detroit kwenda Vegas kwahiyo kufika Amsterdam nilimiss flight ya connect Amsterdam kwenda detroit kwa hiyo ikabidi ni rebook booking yangu ili nipate flight nyingine ya kwenda Las Vegas kwa hiyo nikakosa connection ya kwenda detroit nikapata connection nyingine ya kupitia Minnesota nilivyofika kule wakati nimefika airport ndege ambayo nilipata connection na hii ya pili ikawa tayari ilikuwa imenichelewesha kwasababu ilikuwa inatakiwa inifikishe siku ya show sasa pale kukawa na tatizo kule watu wa venue siku ambayo waliokuwa wameongea nao
kwa hiyo ikabidi waongee kuwa msanii amechelewa lakini tunaomba event tufanye siku nyingine lakini wale jamaa wakakataa wakasema haiwezekani na lengo ilikuwa mimi ni perform kwenye hiyo weekend ya ruby kwa hiyo kutokana na mazingira hayo ikabidi wale watu wa immigration unajua siku zote ukifika ile ni nchi unavyoingia siku zote lazima kuna maswali ya security pale lazima uulizwe, unajua watu hawajui kitu kimoja kwamba kupata visa sio ndio kuingia kwenye nchi ya mtu kwamba ukifika nchi yoyote hata sisi tunaenda South Africa naona ni nchi ambayo tunaingia bila visa ukifika airport lazima uulizwe unakuja kufanya nini, unakaa siku ngapi, kwa hiyo nchi zote utaratibu ndio huo kwa hiyo katika pale kuulizwa nikawambia naenda Las Vegas kwenye show, kwa hiyo mara nyingi unajua wa marekani ni watu wakutaka kujiridhisha au hata hapa Tanzania wageni wanakuja unaweza ukamuona Mzungu, Mhindi, Mwarabu, mtu mweusi akifika pale kwenye passport control lazima wahusika wa hapo airport wajiridhishe pengine hata wapige simu kwa huyo mwenyeji wako, kwahiyo wakapiga simu kule kwa watu wa event pamoja na sehemu ya Venue kwa hiyo watu wa Venue wakaambiwa kulitakiwa kuwe na show ila msanii hakufika kwa hiyo wakabidi waongee na promote akasema tumeisongeza kwasababu msanii amechelewa amemiss flight sasa wakarudi kwangu wakaniambia lengo lilikuwa uje kwenye hii show na show tayari umeshaimiss kwasababu ya matatizo ambayo sisi hatutakiwa kuyajua yamesababishwa na nini wakasema kwamba lakini hapa inaonesha una show nyingine New york tarehe 21 nikawaambia ndio nilikuwa ninayo ila nilipanga nikitoka Las Vegas naelekea huko. 
Wakaniambia sasa hii show ndio tunatatizo nayo kwasababu ni show ambayo inahusisha chama cha kisiasa na kama uliona hata kwenye promotion yangu nilikuwa nimeandika kuwa nitakuwa na show ya miaka 38 ya CCM Marekani, unajua vyama cha siasa hivi Chadema, CCM wanamatawi yao kule Marekani watu wanaoishi nje mara nyingi uwa wanafanya sherehe sherehe za Annivesary , kwa hiyo wakaniambia kuwa hii visa yako haikuruhusu wewe kuperform kuna aina ya Visa ya inayoruhusu msanii ku perform kwasababu show yako ni kama ya kisiasa, kwa hiyo kwa kuangalia hivyo wakaniambia option iliyopo itabidi nirudi nyumbani kwasababu shughuli iliyokuleta imeshindikana kwa hiyo unaweza ukaja mwenyewe baadae kwa matembezi yako au kwa nini lakini hata ikitokea mfano leo nikakatiwa ticket au nikate ticket nirudi Marekani visa yangu sasa hivi hainiruhusu kwa hiyo ina maana ninataka kuchukue visa nyingine yenye kibali maalumu chenye kuperform mimi kwenye show, na kama ukivunja sheria zao wanaweza wakakufungia miaka mitano halafu wanakupiga faini dola elfu 1o kwa hiyo mimi mwenyewe nikakubali lazima pia uangalie mazingira na mimi lazima nitengeneze mazingira yangu ya kazi kwa hiyo nikawaambia sawa nitarudi nyumbani kwa hiyo nasubiri tu sasa hivi wale promote wa show ya Las Vegas wapange kwaajili ya venue ya show nyingine then nitaendelea na mchakato mwingine kama kawaida. 
Millardayo…: ‘ilikuwaje mpaka unamiss Flight? Ommy Dimpoz: unajua kumiss flight kunatoka hata hapa Dar unaweza ukamiss flight, unajua nilishazoea kukaa kwenye zile connection za masaa matatu reporting time kwahiyo nilijichanganya kwenye masaa halafu ukishaondoka hivi inakuwa kidogo hivi masaa yanazigua kwa hiyo inabidi uwe makini kidogo kwa hiyo katika kuangalia pale yaani mimi fikra zangu na mawazo na nilishazoea zile flight za kuunganisha labda za kwenda DC unaweza ukakaa pale masaa matatu au masaa matatu na nusu kufanya connection ya kwenda lakini ile ilikuwa na connection ya muda mfupi kama lisaa limoja kwa hiyo mpaka ushuke, utoke sijui geti unalotakiwa kwenda kwahiyo katika mishe mishe nikakuta ile flight mlango umeshafungwa kila kitu wakasema haiwezekani na hata begi langu walikuwa wamelishusha kitu kingine nimeshazoea kama mule uwanja unataka watu wanatangaza kwasababu ilishawahi kunitokea mara nyingine labda unakuta abiria amechelewa flight kwasababu sisikii tangazo lolote nimekaa angani kama almost masaa tisa nafikiri nane kutoka Dar kwa hiyo nilipofika nikaunganisha wifi nikawa nimepata internet nikaingia ghafla kwenye whtsspp nasoma SMS nawaambia washikaji wa kule marekani kuwa nakuja nimeshafika Amsterdam kitendo cha pale kuchati kuwa wish watu valentine nakutana flight imeshaondoka. 

Millardayo…: ‘Baada ya wao sasa kukuambia unarudi Tanzania yaani uligeuzia pale pale Airport au mazingira yalikuwaje?.. 

Ommy Dimpoz…;“Waliniweka Hotel kwa sababu hiyo flight ilikuwa ni ya siku inayofata ambayo ni jioni mpaka zile ndege zinavyotoka huku zifike Amsterdam, zifike pale kwa hiyo ilikua ni siku inayofata.
-millardayo
[Continue Reading]

Wednesday, May 21, 2014

Kwa Staili Hii Diamond Badilika Kabla Mambo Hayajaharibika..Kwa Mengine Hongera.

Mwaka 2014 umekuwa ni mwaka wenye neema nyingi kwa Diamond Platnumz kimataifa. Tangu aachie video ya remix ya My Number One aliomshrikisha Davido, jina la staa huyo limekuwa kubwa kiasi cha sasa kumfanya afike sehemu ambayo hakuna msanii wa Tanzania aliyewahi kufika.

Kuanzia video yake kushika namba moja kwenye vitu vikubwa vya TV kikiwemo Trace TV, kutajwa kuwania tuzo za MTV MAMA katika vipengele viwili na pia kutajwa kuwania tuzo za BET kwenye kipengele cha Best International Act: Africa. “An international music superstar from Tanzania is being born right before our eyes. Hongera sana @diamondplatnumz,” alitweet January Makamba.

Ni kweli, supastaa wa kimataifa kutoka Tanzania amezaliwa mbele ya macho yetu na ni wajibu wetu kumuunga mkono katika kila hatua anayoenda. Lakini kama unamtakia mtu heri na mafanikio zaidi, si lazima kumsifia muda wote. Ni vyema kumwambia ukweli pale ambapo tunahisi anatakiwa kuparekebisha ili asonge mbele zaidi.

Jambo muhimu ambalo Diamond anatakiwa kurekebisha ni katika live performance. Naomba nikiri kuwa pamoja na kuwa shabiki mzuri wa nyimbo nyingi za Diamond, sijawahi kupenda performance zake za live. Nimeshamhudia kwa zaidi ya mara 10 akitumbuiza na zote nimekuwa nikimuona akifanya vilevile na sipati kile ambacho nakuwa nakitegemea.

Juzi alikuwa mmoja wa wasanii waliotumbuiza kwenye show ya Road to MAMA ya MTV Base iliyofanyika Club Bilicanas akiwa pamoja na Sauti Sol na kundi la Mi Casa Music. Bahati mbaya ama nzuri kwake ni kwamba kutokana na kuwa msanii mwenyeji, yeye alikuwa msanii wa mwisho kutumbuiza. Walianza Wakenya Sauti Sol ambao kwa mtu aliyekuwa pale ukumbini atakubali kuwa show yao ilishangiliwa sana

Baadaye walifuata Mi Casa Music na wao wakadhihirisha kwanini ni kundi bora la muziki wa house kwa sasa nchini Afrika Kusini kwa kupiga show kali sana.

Diamond alifuata na kama kawaida wakati anaingia alishangiliwa mno. Kama kawaida yake, aliungana na dancers wake wanne waliokuwa wakimpa support. Ilikuwa show ya kawaida iliyoboa kwa muda mfupi tu.

Ushauri wangu kwa Diamond ni kuwa asiconcentrate sana katika kucheza na kusahau kujiimarisha katika uimbaji wa live. Haoneshi ujuzi wowote wa kuziimba nyimbo zake kiustadi anapokuwa stejini. Kwakuwa hujikuta akicheza mno na hivyo kuchoka haraka, sauti yake huharibika na kusikika vibaya na huondoa kabisa ule uprofesheno wa sauti ya msanii anayependwa na mwenye hits nyingi. Kama angekuwa anaimba na vyombo live show ingekuwa inapewa jeki na muziki tofauti unaopigwa na bendi.

Atafute namna nyingine ya kiubinifu zaidi ya uimbaji wa nyimbo zake live. Asitumbuize nyimbo kama zinavyosikika kwenye CD. Kama ataendelea na performance za kutumia DJ na CD, basi atengeneze version tofauti za beats atakazotumia kuimba live. Madhara ya hiki anachokifanya sasa ataonekana kama dancer badala ya kuwa muimbaji, sifa aliyonayo Cabo Snoop.

Kelele na shangwe anazozipata akiwa anatumbuiza zisimdanganye kuwa anazikonga nyoyo za mashabiki kwa performance kali kwakuwa ukweli ni kwamba shangwe nyingi ni kwasababu nyimbo anazoimba ni hits na wengi wanazifahamu. Kwa perfomance ya aina ile kama angekuwa ni msanii asiye na jina, wengi wasingekuwa wanarespond hivyo.

Shabiki hapendi kwenda kumuona msanii ambaye nyimbo zake hutumbuiza nyimbo zake vilevile kama zinavyosikika redioni. Kwa walioshuhudia show ya P-Square November mwaka jana pale Leaders Club waliona jinsi mapacha hao walivyo wachawi wa live performance.

Pamoja na kuwa wachezaji wazuri, hawakuwa wakicheza katika kila wimbo. Muda mwingi walikuwa wakiimba nyimbo zao kwa hisia na kuinteract vizuri na watazamaji.

Kwakuwa kutajwa kwake kwenye tuzo hizo kubwa kutampa exposure zaidi na kupata show za kimataifa, alifanyie kazi hilo ili kutowapa sababu wakosoaji na kumuona kama amebebwa tu kufika hapo.
Bongo5
[Continue Reading]

Sunday, May 11, 2014

P Square – Taste the Money (Testimony) [Official Video]


[Continue Reading]

SOMA HAPA HISTORIA FUPI YA DOUBLE BRAIN MCHIZI ANAEMILIKI ROCK TOWN RECORDS YA JIJINI MWANZA

Hii ndio historia kutoka kwa Hamidu Salum aka Double Brain kutoka pande za Mwanza baada ya kufunguka kupitia ukurasa wake wa facebook
Mkubwa Hermidou


KUKUMBUSHANA NI KITU MUHIMU SANA. nimezaliwa Kinondoni mkwajuni, shule ya msingi nimesoma Mwongozo kinondoni, shule ya sekondari(o'level) nimesoma Kambagwa kinondoni nilikuwa maarufu kwa jina la Double Brain, A'level nimesoma Tegeta pia maarufu kama Double Brain au Hammy Brain, chuo CBE Mwanza, niliingia Mwanza tangu mwaka 2010 mwishoni, sasa natumia jina laMkubwa Hermidou lakini jina langu halisi ni Hamidu Salum, wimbo ambao nimeachia kwa sasa unaitwa NDOTO ZA MKEO ni audio na video, but nilishawahi kufanya nyimbo tofauti kipindi cha nyuma kama mwanaharusi nilifanya SEI RECORDS producer SEIBLAST, nilifanya party party nikiwa na Dar crew pamoja na Juma Nature pale Backyard production chini ya producer ambaye sasa ni marehemu Complex( R.I.P), nilifanya wapi wazazi na Hammer Q Serious record producer Effector, nilifanya pilika pilika na Oxy G pale Midman record, nilifanya bang pale pamoja record producer Nas B nilimshirikisha Becka Title, pia nilifanya ngoma nyingine palepale pamoja record nikiwa na Kiba gitta au drama pamoja na Mc Power, kwa J SILK nilifanys ngoma na Oxy G, Vunja record nilifanya remix ya wapi wazazi na Barakah DA Prince, na kaxi nyingi nimefanya kwenye studio yangu ROCK TOWN RECORDS ambako wanamuziki wengi wenye majina wamepiga na wanaendelea kupiga kazi zao, MUNGU TUBARIKI.
 
[Continue Reading]

Tuesday, May 6, 2014

SOMA HAPA KUJUA ALICHOSEMA MSANII FID Q BAADA YA KUPATA TUZO


Kupitia ukurasa wa facebook leo msanii anaewakilisha pande za Mwanza Mwanza Fid Q afunguka haya baada ya kupokea tuzo mbili kwenye music kili awards

Kwema wakubwa wa kazi!!??
Hakika KTMA wamemfurahisha kila mtu mwenye nia nzuri na huu mziki wetu ( ndani na nje ya Tanzania ) kwa uamuzi huu.. Na ndio maana mwaka huu wamevunja rekodi ' ya kutolalamikiwa na mtu yeyote '
[Continue Reading]

Thursday, March 13, 2014

"RAFIKI WA KWELI UTAMJUA TU KWENYE MATATIZO SIYO WALE WANAFIKI WALIYONIKIMBIA KWENYE SHIDA" RAY C

STAA nguli wa muziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila,’’Ray C’ amefunguka kuwa alipopata matatizo kipindi alipokuwa akitumia madawa ndipo alipogundua rafiki wa kweli na wa uongo ambapo wengi aliowachukulia kama ndugu ndiyo walikuwa wa kwanza kumkimbia na wale aliokuwa akiwategemea ndiyo waliokuwa mstari wa mbele kumsaidia japo kwa ushauri.
Kupitia account yake ya instagram Ray C aliandika ‘’Nilipopata matatizo ndio niligundua rafiki wa kweli na rafiki waongo kwani wengi niluowachukulia kama ndugu ndio walikuwa wa kwanza kunikimbia na wale niliokuwa nisiowategemea ndio walikuwa mstari wa mbele kunisaidia japo ushauri.
Usiyemdhania ndiye…..wanaokuumiza ni wale walio karibu yako siku zote so guys be very careful na watu wa karibu wanaojua kila kitu chako! na hao ndio wanaoweza hata kukudhuru..
[Continue Reading]

Wednesday, March 12, 2014

New Music: Baraka da Prince ~ Jichunge


[Continue Reading]

KUMBE THE LATE ALBERT MANGWEA ALIWAHI KUMKATAZA PRODUCER MSWAKI KUTUMIA STYLE YAKE

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh0eOxXtLr7X52vw-Nt-yaz3A95OMDR1n2c-wb1_ScfuUWT2b2NXXx6JFPqOjFOLq43znqDDqGwZ6AT608lMn3C1Kw255UwtEfCymR2VyUoN1oEd1h6pHXph3s8RXEidzgwK634eZcmQyQF/s1600/Albert+Mangwair.jpgKWA WAKATI HUU THE MULTI TALENTED PRODUCER AMBAYE PIA NI RAPPER CEO WA BLACK CURTAINS RECORDS, ANA PROJECT INAITWA KEEPING NGWAIR ALIVE, ITAKUA NI ALBUM YENYE NGOMA KADHAA, NA YEYE MSWAKI ANA RAP KWA KUTUMIA STYLE YA ALBERT MANGWEA, TAYARI AMESHA RELEASE NGOMA MBILI MOJAWAPO NI OPEN LATER NA NYINGINE INAITWA GHETTO AMEI RELEASE HIVI KARIBUNI
JE NGWEA ANGEKUA HAI ANGERAP KWA STYLE HIYO?
MSWAKI PIA AKAZUNGUMZIA MPANGO WAKE WA KWENDA KUPATA BARAKA ZA MAMA ALBERT, KABLA YA KUIFANYA PROJECT HIYO KWA UKUBWA ZAIDI
MSWAKI ANAONDOKA KESHO KUELEKEA MOROGORO KWA KINA NGWEA, SWALI JE, MSWAKI ATAKUBALIWA KUFANYA ANACHOKIFANYA KUTOKA KWA FAMILIA YA THE LATE ALBERT MANGWEA?
CREDIT : PERFECTTZ
[Continue Reading]
Powered By Blogger · Designed By Seo Blogger Templates