Monday, January 2, 2017

KIPA WA SIMBA ALIVYOCHAFUA DAFTARI


Golikipa wa Simba Daniel Agyei ameruhusu nyavu zake kutikiswa kwa mara ya kwanza tangu alipojiunga na klabu hiyo katika dirisha dogo la usajili kuchukua nafasi ya Vicent Angban ambaye baadae alitemwa kwa kile kinachotajwa kuwa ni kiwango kidogo.
Agyei amecheza mechi tatu za ligi kuu Tanzania bara (Ndanda  FC 0- Simba, Simba 1-0 JKT Ruvu na Ruvu Shooting 0-1 Simba) na akifanikiwa kutengeneza clean sheets kwenye mechi zote. Alicheza pia mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya Mtibwa Sugar (haukua mchezo wa mashindano rasmi) na kumaliza dakika 90 akiwa ameruhusu magoli mawili Simba ilipoteza kwa kufungwa 2-1.
Goli alilofungwa golikipa huyo kutoka Ghana lilitokana na kona ambapo beki wa Simba Novat Lufunga alijifunga wakati akipambana kuokoa mpira.
Kwahiyo Agyei ameruhusu goli moja hadi sasa katika mashindano rasmi yanayotambuliwa na TFF ukiondoa mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo aliruhusu magoli mawili katika kipigo cha Simba 1-2 Mtibwa Sugar.
Chanzo: http://shaffihdauda.co.tz/2017/01/01/golikipa-wa-simba-amechafua-daftari/

No comments:

Speak Your Mind

Powered By Blogger · Designed By Seo Blogger Templates