KUKUMBUSHANA NI KITU MUHIMU SANA. nimezaliwa Kinondoni mkwajuni, shule ya msingi nimesoma Mwongozo kinondoni, shule ya sekondari(o'level) nimesoma Kambagwa kinondoni nilikuwa maarufu kwa jina la Double Brain, A'level nimesoma Tegeta pia maarufu kama Double Brain au Hammy Brain, chuo CBE Mwanza, niliingia Mwanza tangu mwaka 2010 mwishoni, sasa natumia jina laMkubwa Hermidou lakini jina langu halisi ni Hamidu Salum, wimbo ambao nimeachia kwa sasa unaitwa NDOTO ZA MKEO ni audio na video, but nilishawahi kufanya nyimbo tofauti kipindi cha nyuma kama mwanaharusi nilifanya SEI RECORDS producer SEIBLAST, nilifanya party party nikiwa na Dar crew pamoja na Juma Nature pale Backyard production chini ya producer ambaye sasa ni marehemu Complex( R.I.P), nilifanya wapi wazazi na Hammer Q Serious record producer Effector, nilifanya pilika pilika na Oxy G pale Midman record, nilifanya bang pale pamoja record producer Nas B nilimshirikisha Becka Title, pia nilifanya ngoma nyingine palepale pamoja record nikiwa na Kiba gitta au drama pamoja na Mc Power, kwa J SILK nilifanys ngoma na Oxy G, Vunja record nilifanya remix ya wapi wazazi na Barakah DA Prince, na kaxi nyingi nimefanya kwenye studio yangu ROCK TOWN RECORDS ambako wanamuziki wengi wenye majina wamepiga na wanaendelea kupiga kazi zao, MUNGU TUBARIKI.
No comments: