Saturday, November 30, 2013

WINGI WA MAGARI KWENYE MAHAFALI YA CHUO KIKUU ST'AUGUSTINE MWANZA.WENYE MAGARI WALAZIMIKA KUTUMIA NJIA ZA VICHOCHORINI KUKWEPA FOLENI NJIA YA KUINGIA MWANZA MJINI

Hali katika Jiji la Mwanza leo ilikuwa mbaya sana kwa watumiaji wa barabara.iendayo nyengezi,buhongwa,mkolani nk kutokana na wingi wa magari yatokayo mjini na ata magari yanayoingia kutoka mikoani kuingia Mwanza mjini kuwa na wingi wa magari yaendayo Chuo Kikuu cha St Augustine Mwanza maarufu kama Malimbe.Wingi magari leo katika Jiji la Mwanza kumesababishwa na magari yaliyo mengi kuelekea Chuo kikuu hicho cha Mwanza kwenye Mahafali ya Wanachuo waliokuwa wanahitimu elimu yao ya juu kwenye Chuo hichoi..Hali iliyosababisha magari kutumia barabara za pembeni kuepuka foleni kubwa kuelekea.Mwanza mjini.mpaka tunaripoti habari hii hali ya foleni imepungua nyakati za jioni baada ya ndugu kuondoka na wanachuo wao.hali iliyopelekea kupungua kwa magari kwenye barabara kuu ziingiazo Jijini Mwanza...

No comments:

Speak Your Mind

Powered By Blogger ยท Designed By Seo Blogger Templates