Wednesday, December 3, 2014

Fahamu kwanini watu wengi hupoteza hamu ya kujamiiana..Soma Hapa


Katika utafiti uliofanyika miaka ya karibuni nchini Marekani, imebainika kwamba kati ya ndoa 6,000 zilizovunjika, asilimia 57 zimesababishwa na mwenza mmoja au wote kupenda kuchati au kutumia intaneti kupita kiasi na hivyo kusababisha msisimko kupotea kati ya wenza wawili na hatimaye mwisho ni kupungua uwezo au hamu ya kujamiana.


Ni kundi gani la wanawake lililo katika hatari ya kukumbwa na tatizo hili?

  1. Wanawake ambao wana historia ya kupungua hamu ya kujamiana
  2. Wale ambao wamefanyiwa upasuaji wa kuondoa mayai yao ya uzazi kutokana na sababu mbalimbali
  3. Wanawake waliofika umri wa kuacha kupata hedhi (miaka 42-58)) na kupata dalili mbalimbali kama kutokwa na jasho usiku, kukosa usingizi mzuri na msongo wa mawazo.

Kwa wanaume, visababishi vya tatizo la kupungua hamu au uwezo wa kujamiana ni kama ifuatavyo;

  1. Msongo wa mawazo kama nilivyoeleza hapo juu. Kupungua au kukosekana upendo/mapenzi katika uhusiano/ndoa.
  2. Unywaji pombe kupindukia kama nilivyoeleza awali.
  3. Utumiaji wa dawa za kulevya
  4. Uvutaji sigara - Hupunguza kiwango na uzito wa mbegu za kiume.
  5. Uzito wa mbegu za kiume hupungua kwa asilimia 22-57 kwa wale wanaovuta sigara. Uwezo wa mbegu za kiume kuogelea kwenye mirija ya uzazi ya mwanamke pia nao hupungua kwa asilimia 20 kwa wale wanaovuta sigara ikilinganishwa na wale wanaume wasiovuta sigara.
Utafiti mwingine umethibitisha kuwa wanaume wanaovuta sigara wana asilimia kubwa ya kutoa mbegu ambazo hazina maumbile mazuri au ya kawaida na hivyo kuongeza uwezekano wa mimba kutoka au kuzaa mtoto mwenye maumbile ambayo siyo ya kawaida.

Tafiti mbalimbali pia zimethibitisha kuwa uvutaji sigara huharibu mirija ya seminiferous tubules ambayo hupatikana kwenye korodani na ni sehemu ambapo mbegu za kiume hutengenezwa, hivyo uharibifu wake hupunguza wingi na uzito wa mbegu
Pia uvutaji sigara hupunguza vichocheo aina ya testerone, growth hormone, na vinginevyo.
Wanaume wenye kiwango kidogo cha testerone huwa na tatizo la kupungukiwa uwezo wa kujamiana na kiwango kidogo cha mbegu.

Uvutaji sigara hupunguza mzunguko wa damu unaopita/ kwenda kwenye moyo na kwenye uume na hivyo basi kumfanya mwanamume kushindwa kusimika na kupata tatizo la kupungua uwezo wa kujamiana.

Katika tafiti zilizofanyika, asilimia 97 ya wale waliogunduliwa na tatizo hili walikuwa wavutaji sigara na katika tafiti nyingine asilimia 87 ya wale wenye tatizo hili walikuwa pia wavutaji sigara.
Katika utafiti uliowahusisha wapenzi 290 mwaka 1999, ilionyesha kwamba wanaume ambao walikuwa wavutaji sigara walifanya tendo la ndoa na wake zao mara 6 tu kwa mwezi mzima na wale ambao hawakuwa wavutaji sigara walifanya tendo la ndoa mara mbili zaidi ya wale wavutaji sigara.

Uvutaji sigara, huhusishwa pia na kuongezeka kwa chembechembe nyeupe za damu kwenye mbegu za kiume ambazo kwa kawaida hutolewa kukiwa na ugonjwa ndani ya mwili.

Chembechembe hizi ambazo zinakuwapo kwa wingi kwenye mbegu za kiume pasipo na kuwapo kwa ugonjwa, hupunguza uwezo wa mbegu kuingia na kuungana na yai kutoka kwa mwanamke na hivyo kusababisha kutotunga kwa mimba.

1. Ugonjwa wa kisukari
2. Uzito uliopitiliza unaotokana na kuongezeka kwa mafuta ambayo husababisha mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye moyo na uume kuwa midogo na kupungua uwezo wa kujamiana.
Kupungua uwezo wa kujamiana au kufanya mapenzi kwa wanaume ni ishara mojawapo ya ugonjwa wa moyo na kiharusi. Matatizo ya vichocheo katika tezi la koo

  • Kuwa na wasiwasi.
  • Kupenda mitandao ya kijamii kupita kiasi .
  • Umri - Kuanzia miaka ya 40, kiwango cha kichocheo aina ya prolactin huongezeka na kusababisha kuongezeka kwa kichocheo kingine aina ya dihydro-testerone ambacho husababisha tezi dume kuongezeka na hatimaye kupunguza uwezo wa kusisimka kwa mwanamume.
  • Madhara katika neva inayohusika na kusimika kwa uume
  • Kuendesha baiskeli muda mrefu (kwa kipindi kimoja) - Hii hugandamiza neva na mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye uume na kusababisha tatizo la kupungua kwa nguvu za uume.

No comments:

Speak Your Mind

Powered By Blogger · Designed By Seo Blogger Templates