Thursday, May 15, 2014

FAHAMU SABABU 10 ZA WANAWAKE WENGI KUACHIKA MAPEMA SIKU HIZI


1) Kwanza kabisa ni wavivu kwenye swala zima la mahaba, eti wanadai wamechoka na mihangaiko akirudi nyumbani yeye anakula tu kisha analala, hapo ujue ndio haamki mpaka asubuhi akitaka kwenda kazini.

2) Hawajitumi, atakavyo kaa ndio hivyo hivyo mpaka mwisho wa mchezo, haangaiki wala hajihangaishi.

3) Akishapata tu kazi ndio balaa kabisa anakuwa busy na kujifanya amechoka kama anaumba watu.


4) Kama mume wake hajisikii yeye pia hajisikii, yani hawezi kumleta mumewe kwenye mood ya mapenzi hajisumbui kufanya utundu kwani nae anajiona yuko juu hana huo muda
5) Siku zote anasubilia yeye aanzwe , yeye kuanza hataki . Yani mpaka uanze kumchezea na kumuimbisha kama vile demu mpya kumbe mkeo.

6) Akipata pesa yeye hizo ni za kwake na matumizi yake tu binafsi, majukumu kwenye familia yeye hataki keshajitoa, pesa za mwanaume ndio zitumike hadi kumnunulia pedi zake.

7) Wanamaneno mengi hadi muda mwengine huwakosea heshima waume zao, mwanamke kuongea sana haipendezi. Mwengine ukimkuta anaongea na mume wake utafikiri anaongea na konda

8) Wanajali marafiki zako kuliko hata waume zao wa ndani

9) Mitandao ya kijamii inawaponza sana dada zetu, ndoa zina vunjika kila siku. Wala hakuna cha maana niumbea tu na kupost picha kila muda instagram na facebook. wewe umeshaolewa huko instagram unampostia nani,na  ili iweje.

10) Kuzurula, mwanadada unakuta anazurula utafikiri anashughuli ya maana, tena bora azurule na atoe taarifa anaenda wapi lakini walaa mwanamke anatembea kama dalali, mara magomeni, mara kinondoni mara mwananyamara mara sinza yani kama vile muuza urembo. mjirekebishe la sivyo mtaachika mpaka mkione cha moto.

No comments:

Speak Your Mind

Powered By Blogger · Designed By Seo Blogger Templates